Nguvu ya Ulimi.

By | May 23, 2016

Wanasema Ulimi ni kiungo kidogo sana lakini kinaweza kufanya mambo makubwa.
Ulimi unaweza kuvunja ndoa yako.
Ulimi unaweza kukukosanisha na ndugu jamaa na marafiki.
Ulimi unaweza kukupeleka jela.

Ulimi unaweza kujenga mahusiano mazuri na watu.
Ulimi unaweza kukupatia kazi nzuri sana.
Ulimi unaweza kubadilisha maisha yako Leo.

Unatumiaje kiungo hiki ili kupata manufaa zaidi kwenye maisha yako?
Unazungumza nini juu ya maisha yako mwenyewe? Kile unachojinenea ndio kinatokea kwenye maisha yako.

Ukiamka asubuhi ndio nafasi ya pekee kutumia kiungo hiki kujinenea mambo makubwa juu ya maisha yako.
Jiambie, mimi ni mshindi, mafanikio ni ya Kwangu,  siku ya Leo nakwenda kupata kila ninachokitaka, mimi ni tajiri,  anza kujinenea yale yote unayotamani yatokee kwenye maisha yako. Ndoto zako na malengo yako jinenee yote. Kila siku asubuhi.

Ubongo wako utachukua yale unayojinenea na utafanya vitokee kwenye maisha yako. Utajikuta unavutia kila aina ya mafanikio kwasababu vile ulivyojinenea vimekaa kwenye Ubongo wako.

Maisha yako yataendelea kua magumu kama kila siku unatumia Ulimi wako kulalamika na kulaumu. Ukisema maisha magumu, kwetu ni masikini itakua hivyo hivyo maana maneno hayo yanaenda kujijenga kwenye Ubongo wako na matokeo utayaona kwenye maisha yako.

Anza leo kutumia kiungo hiki ubadili maisha yako kuna nguvu kubwa sana juu ya maneno unayojinenea.  Tumia vyema ujipatie matokeo bora kwenye maisha yako.

Ulimi unawagombanisha watu na ulimi huo huo ndio unawaunganisha waliogombana.

Tumia vyema kiungo hiki cha ajabu .

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Mwandishi  Kocha wa Mafanikio na Mjasiriamali.

www.jacobmushi.com/huduma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *