Heri ya Mwaka Mpya Rafiki, Wakati tumeanza leo mwaka mpya napenda ujiulize swali moja la muhimu sana. Je ni nini chanzo cha ndoto zako? Unafahamu ndoto zako zimetoka wapi?

Kuna wengine ndoto zao zimetokana na kukataliwa, kuachwa, kuonekana hawawezi na kadhalika. Maisha yao yote wanapambana ili siku moja waje wawaonyeshe wale waliosema hawawezi kwamba wanaweza.

Kuna wengine ndoto zao ni kama kulipiza kisasi kwa wengine. Kila anachokifanya ni ili Fulani aliemuacha aone kwamba amefanikiwa.

Wengine ni zimetokana na watu ambao wanaushawishi mkubwa kwao.
Wengine ni wazazi wao waliwaambia kwamba wewe unafaa sana uwe mtu Fulani.
Je ndoto yako inatokana na nini?

Inawezekana hufikii mafanikio kwasababu tu chanzo cha ndoto yako ni tatizo. Umebeba visasi ndani ya moyo wako, umejazwa taarifa ambazo sio sahihi na unaenda nazo bila ya kujua unapokwenda.

Chanzo cha ndoto zako kinapaswa kuwa ni Mungu pekee. Yeye ndie aliekuleta hapa duniani akiwa anajua anataka uje ufanye nini. Kama utashindwa kuwa karibu na Mungu utajikuta unarudia mafanikio ya wengine.

Unaweza kujikuta unaishi ndoto za wengine kwa kuzitekeleza. Rudi kwa Mungu akupe maono yake, na ndoto zako.

Kusudi la Mungu kukuleta wewe hapa duniani ndio limebeba kila kitu kwenye Maisha yako. Ukienda nje ya kusudi unapotea. Na kamwe huwezi kufurahia mafanikio yaliyotoka nje ya kusudi la Mungu.

Kabla hatujafika mbali leo tarehe moja jitafakari tena upya unachokifanya kinatokana na nini? Ni Mungu au ni vitabu ulivyosoma? Ni kusudi lake au ni watu ambao walikuhamasisha?

Tengeneza safari yako Mapema kabla hujafika mbali. Bado hujachelewa.

Nakusihi sana USIISHIE NJIANI.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading