Kama tunavyofahamu kwamba kila kitu kilichopo ndani ya maisha ya mtu ni matokeo ya vitu alivyokua akivifanya huko nyuma, yaani kama una afya  mbovu, kuna uzembe ulifanya  labda hukula chakula bora, hufanyi mazoezi n.k. hivyo hivyo kwenye upande wa kifedha kama kwa sasa una tatizo la pesa ni matokeo ya uzembe ulioufanya muda uliopita. Tuankwenda kuangalia sifa za waliofanikiwa ni mambo gani watu wenye mafanikio makubwa wanafanya ili na sisi tuweze kujijengea tabia hizo ili tufikie kwenye mafanikio makubwa. 

Kama tulivyoona hapo mwanzo chochote kinachoendelea kwenye maisha yako kwa sasa hivi ni matokeo ya vitu ulivyovifanya huko nyuma hivyo basi kama utazifahamu tabia za waliofanikiwa na ukazifanyia kazi utapata matokeo baada ya muda Fulani.
Wanalala muda mchache.
Tunaposema kulala muda mchache ni kwamba unalala muda unaotosha kikawaida unatakiwa ulale usingizi masaa 6 na hapa ni kwamba unalala mapema na kuamka mapema watu waliofanikiwa wanaamka mapema alfajiri kabla jua halijachomoza wanaamka kuzipangilia siku zao na kumshukuru Mungu. Ukiweza kujijengea tabia hii ndani ya siku 21 itakua ni bora kwako na matokeo yake utayaona kwa kawaida saa kumi na moja alfajiri usiwepo kitandani.
Wana Muda wa kujifunza.
Watu waliofanikiwa ndio watu wanaojifunza Zaidi na kila siku kuliko maskini na watu wa kawaida nimekua nakutana na watu wengi wananiambia mara ya mwisho wao kushika kitabu ni walipotoka shuleni unakuta mtu ana miaka 10 hajawahi kupitia kitabu chochote cha kujifunza Zaidi ya magazeti. Sikiliza audio/video za kuhamasisha, soma vitabu kwa maendeleo binafsi jiunge na makundi ya kusoma siku hizi kwenye ulimwengu huu wa teknolojia huhitaji kurudi darasani simu yako unaweza kuitumia kama darasa ukajiunga na makundi ya Whatsapp ukajisomea kila siku, soma bloga zinazoandika maarifa kama hii na nyinginezo nyingi.
Mara zote wanafanya vile vitu ambavyo ni vya muhimu kwa maisha yao
Watu waliofanikiwa wana ratiba wana mipango yao ya siku week mwezi n ahata mwaka, hawapelekwi na matukio kila linalotokea ndio walifanye, wanaishi kwa ratiba waliojitengenezea wao wenyewe. Hata wewe unaweza kua na ratiba ya siku yako week yako mwezi n ahata mwaka ili usiwe mtu wa kuchukuliwa na kila upepo kila mtu anaekukuta huna ratiba na anaweza kukupeleka anapotaka yeye.
Wana ndoto na malengo yao ya mbele.
Kama tunavyosema mafanikio sio hatma ni safari ni kweli hata tajiri wa kwanza wa dunia Bill Gates ana ndoto zake pale alipo ana malengo yake ya miaka kadhaa ijayo. Kama umefika sehemu ukafikri ni mwisho kwako ukafikri tayari umeshapata kile ulichokua unakitafuta upo kwenye hatari kubwa sana ya kuurudia umaskini. Ndio maana hua ninawaambia watu kwamba kama umeshapata kila kitu ulichokua unakitaka maishani mwako upo tayari kufa? Ukiona umeshtuka ujue bado una safari ndefu kuna mambo mengi yakukamilisha umebakiza.
Money is a result, wealth is a result, health is a result,
illness is a result; your weight is a result. We live in a
world of cause and effect.
Pesa ni matokeo, Utajiri ni matokeo, afya bora ni matokeo, ugonjwa ni matokeo, uzito wako ni matokeo, tunaishi kwenye dunia ya visababishi na matokeo. Ukiweza kuzifanyia kazi tabia hizo chache utaanza kuona matokeo mbalimbali kwenye maisha yako. Tutaendelea na kuziangalia tabia nyingine za watu waliofanikiwa.
Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016
Tuandikie 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading