Habari Rafiki, ninayofuraha kukujulisha kwamba Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Watakaofanya mambo makubwa leo hawana siku ya tofauti sana na wewe bali watafanya vitu vya tofauti kwenye siku hii.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“MIMI NI MSHINDI SIKU YA LEO, MALENGO YANGU YANAKWENDA KUTIMIA,
KILA NINACHOKIFANYA NINAFANYA KWA UBORA TOFAUTI NA JANA, SITAISHIA NJIANI HADI NDOTO YANGU ITIMIE, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Daudi alipokuwa mdogo wazazi wake walikuwa wanamtazama kama mtoto. Ilifika wakati hadi baba yake alimsahau wakati ule Samwel alipokuwa anataka kumpaka mafuta.

Kitu cha kushangaza sana ni kwamba Daudi yeye hakujitazama kama familia yake ilivyokuwa inamwona. Walimwona mchungaji wa Kondoo, huenda zile kazi kazi za nyumbani ndio alikuwa anaachiwa na badala ya kaka zake.

Daudi hakujiona kama mdogo alijitazama kama shujaa. Alijiona kama mkombozi, aliweza kumuokoa mwanakondoo midomoni mwa Simba, aliweza kupambana na Dubu.

Kwa mtazamo ule aliokuwa nao ndio ulimwezesha akaweza kupambana na Goliath na kumshinda.

Wewe Rafiki Yangu Unajionaje? Usijione kama jamii inavyokutazama, jitazame na jione kama vile ulivyo ndani na sio nje.

Usijitazame kwa udhaifu ulionao, jitazame kwa kile unachoweza kukifanya vizuri.

Kamwe Usikubali vile wanavyosema wewe ni nani ikakuingia na kuharibu yule mtu shujaa ndani yako.

Changamoto NdogoNdogo ulizoshindwa Zisikufanye ujione wewe ni dhaifu bado wewe ni shujaa.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading