Ni vitu vichache ambavyo havina uchaguzi yaani kama ni kimoja kipo hicho hicho tu.
Ukikosea kwenye kuchagua unakua umebakiza nafasi ya maamuzi. Kwenye maamuzi unaweza kuamua kuendelea na ulichokichagua au kuanza upya.
Wewe kama kiongozi wa maisha yako mwenyewe unatakiwa ujue unapoelekea ni wapi ili uweze kufanya uchaguzi sahihi na maamuzi ambayo yatakufikisha kule unapokwenda.
Kitu cha kipekee sana ni kwamba kila siku mpya ni nafasi yako wewe kuchagua vyema na kuamua vyema ili ubadili maisha yako na ufikie kule unapotazamia kufika. Tumia vizuri kila siku masaa 24 tunayopewa kuchagua na kuamua vyema.
Haijalishi una miaka mingapi au umekosea mara nyingi kiasi gani leo ni nafasi yako ya kuchagua na kuamua vyema na maisha yako yatakwenda kule unapotazamia.
Umechagua kujifunza fanya maamuzi ya kujifunza kila siku. Kaa na watu wanaojifunza kila siku.
Umechagua kufikia ndoto zako amua leo kuondoka kwenye kundi la watu wasio na ndoto zinazofanana na za kwako kwani utafanana nao.
Umechagua kua Tai amua leo kutokuogopa kwenda juu zaidi ya ndege wengine. Amua leo kutokuogopa changamoto zozote utakazokutana nazo.
Chagua vyema. Amua vyema.
Maisha yako Hayatakua kama yalivyokua.
Karibu sana.
Mushi Jacob