Ni masaa mengine 24 yakwenda kutengeza ndoto zako.

Ni masaa mengine 24 yakwenda kuongeza thamani kwa wengine.

Ni masaa mengine 24 yakwenda kufanya kile unachokipenda.

Ni wakati wako sasa kuamua kwamba unaitumia kila siku vyema ili kufikia yale ambayo umeumbwa ili kuyatimiza.

Ni wakati wako sasa wa kwenda kutimiza kusudi la Mungu kukuleta duniani.

Ni wakati wako sasa kwenda  kuonyesha kua umekubaliwa Mungu alianza kukukubali wewe ndio maana kakuleta duniani na hadi leo upo hai.

Ni wakati wako sasa kutokuogopa chochote watakachosema na kusonga mbele kwenye hatma ya maisha yako.

Mafanikio, ndoto, malengo,  hatma, vyote hivyo unavyo wewe vipo ndani yako wewe ndio unavimiliki usimwogope mwanadamu mwingine.

Ulizaliwa peke yako na utaondoka peke yako usiwasikilize wanaokwambia huwezi kwani kila kitu Mungu kaweka ndani yako.

Je umekua unasuasua?  Hujatambua ufanye nini ili kutimiza ndoto yako?
Hujaelewa leo ulitakiwa ukafanye nini ili maisha yako yawe bora?
Usisite kuwasiliana nami kwa Mawasiliano yangu.

Karibu sana
Mwandishi: Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading