#SiriYaKuaHaiLeo: 2.Upo hai ili kubariki wengine. 

jacobmushi
2 Min Read
Upo hai leo ili ubariki wengine usikubali kua mtu wa makwazo juu ya wengine.

Usikubali kua mkosoaji kwa kila kitu mtu anachokifanya bali jaribu kua mshauri tia moyo wengine.

Usikubali watu walalamike kua wewe ndio sababu hasa ya kushindwa kwao.

Maneno ya kinywa chako yawe baraka yatie moyo wengine yawainue wengine pale wanaposhindwa.

Mtu akipitia shida na taabu atamani kua karibu yako maana atapata faraja.

Usifikiri kumsaidia mtu ni kumpa pesa peke yake au kumpa vitu hata maneno unayozungumza juu ya kile anachokifanya yana nguvu kubwa sana katika kumsaidia asonge mbele.

Anza leo hujachelewa ndio maana upo hai rebebisha maneno ya kinywa chako leo kua mtu anae tia moyo wengine, anaebariki wengine, maisha yako yatakua ya furaha na baraka.

Unapokua na watu wengi wanaozungumza mema juu yako hiyo ni baraka sana.

Anza kujiuliza leo ni nini watu wanazungumza kuhusu mimi? Jiulize tena hua ninatia watu moyo au ninavunja watu moyo?

Mtu akikuomba mchango na huwezi kumchangia usikae kimya mtie moyo kwamba anaweza kufanikiwa katika lile wazo alilolipata maneno yako yanaweza kua sababu ya yeye kufanikiwa kabisa.

Ili maneno yako yaweze kupata kibali mbele za Mungu yanatakiwa yaanze kupata kibali mbele za wanadamu unaowaona.

Asante sana
jacob Mushi

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading