Tunaiona Dunia Jinsi tulivyo sisi na sio jinsi Ilivyo:

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Tumekua na tabia ya kulalamika na kulaumu sana kwamba dunia ni mbaya, maisha ni magumu, Hali ni mbaya lakini ukweli ni kwamba wakati wewe unalalamika na kulaumu hivyo. Wako wenzako kwenye dunia hii hii na inawezekana kwenye mazingira hay ohayo ya kwako anafurahia maisha na kuiona dunia yenye furaha na Amani. Kila mtu anapitia hali yake kutokana na jinsi maisha yake yalivyo.

Badala ya kulalamika huna kitu Fulani angalia ni vingapi ulivyo navyo umshukuru Mungu kwakua kuna wengine ambao hawana ulicho nacho wewe. Kabla hujaanza kuangalia ni kitu gani huna angalia ulichonacho kwanza kisha anza safari ya kutoka hapo ulipo na kusonga mbele Zaidi.

Ukiweza kuiona dunia vile ilivyo na sio kutokana na hali unayoipitia utaishi maisha yenye furaha sana. Jijengee tabia ya kushukuru kwa kila jambo kwa maana hii itakuwezesha wewe upate mambo mengi Zaidi kwako tofauti na kulalamika. Kama utashindwa kushukuru kwa kidogo ulichonacho utawezaje kushukuru kwa vikubwa.

Anza kujenga tabia ya kushukuru itakuletea matunda makubwa kwenye maisha yako. Hata kama unapitia shida kubwa namna gani ni kweli inauma lakini jizuie usilalamike wala kulaumu.
Wakati wewe unalalamika hakuna kazi wako wanaotafuta japo kua na elimu uliyonayo lakini hawajaweza kupata.

 Wakati wewe unakosa furaha kwa kuona vijana wenzako wanaendesha magari wewe bado uko nyuma yupo mtu amelala kitandani hawezi kutembea huu ni mwaka wa tano yeye anachokiomba kwa Mungu wake ni aweze kusimama atembee basi. Wakati wewe unaona vitu ulivyo navyo havina thamani kuna wenzako wanavitafuta hivyo. Chochote ulicho nacho ukishindwa kukithamini hakuna mtu mwingine atakuja akithamini. Thamini kila ulicho nacho kwa sababu ndio vinakufanya wewe uendelee kuonekana mtu kwenye hii dunia sasa hivi wakati unaendelea kutafuta vizuri Zaidi.

Tunarudi pale pale kwamba usijifananishe na wengine wewe ni wewe na maisha yako na kikubwa shukuru sana kwa vile ulivyo navyo na uanze hatua ya kutoka hapo ulipo upate mafanikio zaidi.
Asante sana Karibu.
Jacob Mushi
Mawasiliano jacob@jacobmushi.com.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading