USIISHIE NJIANI

Unapanda Mbegu Gani?

on

Maneno yetu tunayosema mbele za watu ni mbegu, ipo siku yataleta matokeo. Vile unavyozungumza mbele za watu ndivyo watu wanatafsiri kuwa uko hivyo. Kama maneno ni mbegu basi unavyoyapanda mioyoni mwa watu tegemea matokeo yake siku moja.

Hakuna mbegu ambayo haioti kama imetupwa kwenye udongo ikapata na maji. Chunga sana unavyoropoka mbele za watu maneno yasiyofaa kwani yakuja kuzaa matunda yasiyofaa kabisa.
Zungumza maneno ya kujenga, kutia moyo, kuwapa watu watumaini ili wasonge mbele na ipo siku utaona faida yake.
Kuwa balozi wa habari njema popote unapokwenda na kwa kila unachokizungumza.
Hujui unaezungumza nae leo atakuja kuwa nani kesho, na kwa maneno uliyozungumza kwake yamemfanya akuone wewe ni mtu wa namna gani?
Tengeneza namna ambavyo unataka watu wakutambue na anza kuishi hivyo kila siku.
Andika vile unataka watu wakufikirie ana fanya mambo ambayo yatawafanya watu wakuelewe hivyo. Ni kweli huwezi kuwalazimisha watu wakuelewe unaweza kujikuta unapoteza Maisha yako. Ninachotaka kukwambia kwenye ujumbe huu ni kwamba ishi Maisha sahihi, fanya vitu sahihi.
Usifanye vitu kuwaridhisha watu bali fanya vile moyo wako unapenda lakini vitu ambavyo ni sahihi.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

About jacobmushi

Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Leave a Reply

Your email address will not be published.