Marafiki ulio nao wanachangia kwa kiasi kikubwa juu ya tabia yako, mapato,  na pia  baadae yako.  Kama kuna kitu cha muhimu cha kuchunga na kua makini wakati unachagua ni marafiki.

Marafiki ndio  wanasababisha baadhi ya tabia kwenye maisha yetu. Marafiki wanachangia pia hali uliyonayo sasa hivi. Kama unataka kufika mbali na kua na mafanikio makubwa badili aina ya marafiki ulio nao,  badili aina ya watu unaojichanganya nao kila siku.

Kabla hujabadili angalia ni kitu gani wanachangia kwenye maisha yako? Wanachangia nini katika kufanikiwa kwako? Unaweza kufanya kazi kwa bidii sana lakini watakao kuridisha nyuma ni marafiki zako. Inawezekana na wao wanafanya kazi kwa bidii pia lakini wanakosa UADILIFU, NIDHAMU NA mengine mengi.

Marafiki ulionao leo jiulize kwenye kile unachokifanya wana mchango mkubwa kiasi gani ili kukufanya wewe usonge mbele?  Kama hakuna nakwambia wakimbie haraka sana. Wewe ni msomaji wa vitabu unakaa na watu ambao hawasomi hata kitabu kimoja. Watakuambukiza tabia zao.

Kitu cha ajabu ambacho labda ulikua hukijui tabia mbaya zinaambukiza haraka kuliko tabia nzuri. Itakuchukua muda mrefu sana kujenga tabia nzuri lakini unaweza kuipoteza ndani ya muda mchache. Tabia mbaya zinaletwa na marafiki ulio nao Karibu zaidi.

Una ndoto kubwa usikae na watu wenye ndoto peke yake kaa na watu wenye ndoto kubwa kama zako watu ambao wanaweza kukushauri na kukupa nguvu zaidi ya kusonga mbele zaidi.

Katika watu ambao wanapata athari kubwa ya kua na marafiki wabaya ni Vijana. Vijana ndio wapo kwenye kundi la hatari zaidi kwenye kupotezwa na aina ya marafiki walionao.

Badili hata magroup ya Whatsapp ambayo hayana mchango wowote kwenye future yako. Ukiharibika wewe unaharibika mwenyewe hautaharibika nao. Ukipotea wewe hasara ni ya kwako wewe.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading