Kusudi ni nini?
Kusudi ni ile sababu hasa ya kitu kuwepo. Bila Kusudi kuwepo kwa kitu hakuna maana. Kitu cha kwanza cha kutambua kwenye maisha yako ni upo duniani kwa Kusudi lipi. Ukiweza kutambua na ukaanza kuliishi Kusudi hilo maisha yako yatakua ya furaha.

Mojawapo ya vitu vinavyowafanya watu wasiwe na furaha duniani ni pale wanapotoka nje ya kusudi. Embu jiulize kijiko kikipewa kazi ya mwiko kitaweza? Kijiko hakiweza kusonga ugali. Kipo kwa ajili ya kulia chakula. Ukilazimishia kusongea ugali unaweza kukivunja. Ni muhimu sana kutambua kusudi lako na ukalifanyia kazi utaishi maisha yenye furaha kila wakati.

Bila ya kusudi la kitu kutambulika hicho kitu hakiwezi kua na matumizi. Na hata kikiwa na matumizi yannaweza yasiwe sahihi. Ni sawa na ukanunue suti ya ghali ya baba yako mzazi kwa ajili ya siku ya harusi. Ukampelekea bila kumweleza ni ya kazi gani.  Ukija ukakuta amevaa analima nayo shambani utaanza kumlaumu na kumwambia umenunua ghali sana.
Ukweli ni kwamba ile suti hakujua kusudi lake kwa nini ulimnunulia. Hata ungenunua suti ya bei rahisi kabisa lakini wakati unampa ukamwambia ni ya kuvaa siku ya harusi angeitunza vizuri sana bila kujali ni ya bei gani.
Kusudi ndio linaleta thamani ya kitu.

Tambua kwa nini upo duniani bila kutambua utaishi maisha yasiyo na mwelekeo utafanya vitu vingi bila matokeo au hata ukipata matokeo hutakua na furaha nayo. Inatakiwa kila unachokifanya kiwe kimetoka  ndani yako.
Jitambue wewe upo kwa Kusudi lipi sasa ili uweze kuliishi.

Kusudi halibadilishwi. Huwezi kubadili kazi ya kijiko Tayari kipo kwa kazi yake. Ukibadili kusudi la kitu unaleta uharibifu. Haiwezekani sehemu ya kutolea ikawa ya kuingizia. Huwezi kufanya spika ikawa microphone hata siku moja. Ukiweza kutambua kusudi lako huwezi kuacha huwezi kufikia mahali ukasema me nimechoka naenda kufanya kitu kingine Haiwezekani. Hata kama unapitia hali ngumu kiasi gani kwa sababu ni kusudi lako utavumilia.

Kusudi linakuwezesha uweze kujitambua. Ukifahamu kusudi lako utajitambua vyema sehemu zote na uwezo.

Hakikisha unatambua kusudi lako kuiga hakufai hautafika mwisho.  Acha kufata mkumbo fanya kile ulichoumbiwa duniani.

Asante sana
Jacob Mushi
Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading