Upo tayari kupoteza ulivyonavyo upate vingine?

Rafiki yangu mpendwa ni kwamba kwa chochote kizuri unachokitaka kwenye hii dunia lazima ulipe gharama, kwenye gharama watu hua wanakimbia. Ukitaka mafanikio makubwa kuna vitu inakubidi uviache. Ukae mbali navyo.


 Upo tayari kupoteza marafiki zako ulionao sasa hivi ili uweze kwenda hatua nyingine kuna watu inakubidi uwaache nyuma, upunguze ukaribu wako na wao, sikwambii muwe maadui bali namaanisha mipaka inabidi iongezeke. Na hapa ni kwa wale watu ambao hawapo tayari kwenda na wewe kwenye mafanikio makubwa. Watu hawa usipowaweka mbali na wewe watakua wanakurudisha nyuma na kukukatisha tamaa.  Tafuta watu ambao wamefika kule unapoelekea au wanaoelekea huko. Marafiki wanaolalamika kila wakati, wanolaumu,  wanaosema watu vibaya, wasiopenda kujifunza, wasipenda maendeleo, hao watakupoteza achana nao mara moja.

Tabia, kuna tabia ambazo inakubidi uziache kwa namna yeyote ile. Kama ulikua husomi vitabu inakubidi uanze sasa, tafuta kampani ya watu wanaosoma vitabu jiunge nao na anza kujenga tabia ya kusoma vitabu angalau kwa mwezi usiache kusoma kitabu kimoja. Hapa utaukuza ufahamu wako na kule unapoelekea utakuana uwezo mkubwa, fanyia kazi yale unayojifunza kila siku. Acha tabia za kulalamika na kulaumu, kusema watu vibaya, kupoteza muda, kufuatilia vitu visivyo na manufaa kwenye maisha yako. Ukiweza kufanya hivyo utapiga hatua kubwa.

Kwenye kupoteza vitu ndio pakua pagumu maana unakua upo na marafiki wa muda mrefu sana ukiwaangalia mmetoka mbali. Ukishindwa kufanya maamuzi itakua ni hasara kwako maana utakua kama wao milele, tabia ulizozijenga tangia utotoni unatakiwa ukubali kuziacha kabisa.

Kua tayari kupoteza ili upate vya thamani zaidi.
Nikutakie weekend njema.

Asante sana na Karibu
Jacob Mushi 2016
Niandikie 0654726668 Whatsapp, na Email jacob@jacobmushi.com

jacobmushi
Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.