#USIISHIE_NJIANI: Tarajia Makubwa

By | October 2, 2017

Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu?

Kile unachokitarajia ndio kinatokea kwenye Maisha yako. hii ni sharia ya asili ambayo inaongoza maisah yetu. Kama unataka chochote  na tayari umeshajenga picha kubwa ndani yako. Tayari umeshaanza kuifanyia kazi picha hiyo kubwa anza kutarajia matokeo makubwa.

Ondoa wasiwasi juu ya kile unachokitaka. Anza kujitabiria na utarajie kile unachokitabiria. Usikubali kuwa na mawazo yaliyo kinyume na kile unachokitaka.

Ndio ni kweli huwezi kupata kabisa kama ulivyotarajia lakini embu jiulize ukitarajia mabaya tu kwenye kila unachokifanya unategemea kupata mazuri?

 

Kwa kutarajia mazuri na makubwa unajitengenezea njia za kuyafikia. Ukitarajia mafanikio kwenye njia zote za Maisha yako utayaona mafanikio.

Tarajia mazuri kwenye kila unalofanya. Unapoamka asubuhi tarajia kuwa na siku yenye matokeo bora. Tarajia kila jambo zuri unalotaka litokee.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *