Habari rafiki. Utakula matunda ya kile unachokizungumza kwenye midomo yako. kile unachojinenea kila wakati ndio utakula matunda yake.

Hakuna jambo ambalo unazungumza lisitokee tatizo ni kwamba wakati linatokea unakuwa umeshasahau kama ulishajinenea.

Nionyeshe mtu mwenye mafanikio anaelalamika, hakuna mtu wa namna hiyo. Kwanza hana huo muda wa kulalamika.

Vile unavyojisemea unavyojitamkia ndivyo utakavyokuwa.

Anza kubadilisha kinachotoka kwenye mdomo wako toa maneno mazuri kwako na kwa wengine waliokuzunguka.

Kile unachokisema ulimwengu utakurudishia. Ukisema duniani hakuna watu wema tena utakutana na wabaya kila mahali.

Ukisema huu mtaa una wachawi hata ambao hawakuwepo wataanza kuja ili uwaone.

Ukisema wewe ni maskini utawavutia maskini wenzako, na kila unachokifanya kitaleta matokeo ya kimaskini.

Badilisha unachokisema.

Badilisha chanzo cha maneno yako.

Bahati mbaya sana ukishaongea haiwezekani tena kufuta yale uliyosema. Ni vyema ukachunga sana yale unayosema juu yako na kwa wengine.

Ukiona watu unaokaa nao wanatabia za kujisemea mabaya, hali ngumu, Maisha magumu na vitu vingine kaa nao mbali. Ukiona watu unaokaa nao kazi yao ni kusema wengine vibaya kaa nao mbali. Kwasababu hayo ni mbegu unapanda ipo siku zitazaa matunda.

Anza kusema maneno mazuri, sema kile unachotaka kitokee na sio kile usichokitaka. Tengeneza Maisha yako kwa kuyanena vile unavyotaka yawe. Usikubali kukaa na wakatishaji tamaa au waliokata tamaa. Watu ambao wanalalamika kila kukicha, kukiwa na baridi wanalalamika, jua likiwaka wanalalamika, kukiwa na vumbi wanalalamika, kukiwa na tope wanalalamika. Usiku wanalalamika na mchana wanalalamika. Kaa nao mbali watu hawa. Kaa karibu na watu ambao wanapenda kushukuru.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading