448; #USIISHIENJIANI LEO: Ipo Ndani Ya Uwezo Wako.

jacobmushi
1 Min Read

There is nothing happens to any person but what was in his power to go through with.-Marcus Aurelius


Hakuna kitu kinamtokea mtu ambacho hakipo ndani ya uwezo wake wa kupambana nacho.Changamoto uliyonayo sasa una uwezo wa kuishinda.
Majaribu ya aina yeyote unayopitia una uwezo wa kuyashinda. Hakuna namna utaletewa jaribu lililozidi uwezo wako.


Kinachofanya uone kama umezidiwa sio changamoto bali ni vile ulivyoruhusu akili yako itafsiri changamoto hiyo.


Anza Kuyaona matatizo uliyonayo ni madogo na utaanza kuona suluhisho. Ukiona matatizo uliyonayo ni makubwa basi na akili yako inaacha kutafuta suluhisho kwasababu umeshaiambia Haiwezekani.


Chochote unachopitia Usikubali kujiambia huwezi. Usiseme hili ni zito sana, ona kwamba unaweza, ona ushindi.


Usikubali kusema chochote kibaya juu yako hasa wakati wa majaribu. Jinenee Yaliyo Mema na pia Kumbuka Mungu hajakuacha yupo na wewe wakati wote.Hivyo basi hupaswi Kuogopa kama Mungu yupo na wewe kwani pale unapotaka Kuanguka atakushika mkono.


Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading