USITAZAME LEO

By | May 14, 2017
Leo vita ni vingi sana,
Leo hakuna mavuno bado.
Leo wanakusema wengi
Leo inaonekana kama ni ngumu sana.
Leo inaonekana kama utakwenda kushindwa.
Leo inakatisha tamaa sana.
Leo unatoka jasho jingi sana.
Leo unatumia nguvu nyingi sana.
Ukitazama leo utakata tamaa
Ukitazama leo utarudi nyuma.
Ukitazama leo utayaona magumu.
Itazame ndoto yako.
Yatazame mazao yakiwa tayari kwa kuvunwa shambani.
Yatazame matokeo ya jasho unalotoa leo.
Yatazame matokeo ya nguvu nyingi unazotumia leo.
Ukitazama ndoto yako utapata hamasa Zaidi.
Endelea kuitazama ndoto yako kubwa hasa wakati wa magumu.
Wakati wa mavuno ni furaha na vicheko.
Sasa hivi upo mwenyewe lakini wakati wa mavuno utakuwa na wengi sana.
Wakati wa mavuno ndio wakati wa kushangilia.
Wakati wa mavuno ndio wakati wakati hasa kelele zinasikika na zinaita watu.
#USIISHIE_NJIANI.
Jacob Mushi.
Mwandishi, Mjasirimali na Mhamaishaji
Simu: +255 654 726 668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com  
jacobmushi.com.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *