Tumekuwa tukiishi kutokana na picha ambazo tumejengewa na wale watu tulio waamini sana. Watu hawa wanaweza kuwa ni wazazi wetu, ndugu zetu, viongozi wet una hata waalimu wetu. Kila mmoja amekuwa akituaminisha kwa jinsi alivyoelewa na kuamini.

Yako mengi yamekuwa ni makossa na yameendelea kufuatishwa hivyo hivyo bila kujali au yeyote kujiuliza hivi hii ni sahihi kweli? Inawezekana uliaminishwa kuwa huwezi kufanikiwa bila ya kuwajua watu Fulani. Inawezekana uliaminishwa kuwa huwezi kufanikiwa bila ya kwenda kwa mganga akupe ulinzi.

Inawezekana uliaminishwa kwamba waliofanikiwa sana wamewaibia watu walio maskini hivyo hadi sasa umekuwa na fikra hizo na zimesababisha usiweze kufanya chochote kwenye Maisha yako. Hujaweza kuchukua hatua yeyote.

Ndugu yangu, dawa ya kutoka hapo ulipo ni wewe kuamua kubadilisha fikra ulizonazo. Uwe na fikra mpya, uache kuamini umelogwa, uache kuamini kuna mtu anakuchukia, uache kuamini kwamba unahitaji kutoa kafara ya binadamu wenzako ili ufanikiwe. Bila hivyo ni sawa na kusukuma ukuta.

Watu wote waliopokea uponyaji kwenye Biblia chanzo cha uponyaji wao kilikuwa ni Imani mpya walizoziingiza kwenye mioyo yao. Kipofu Bathimayo aliposikia Yesu anaponya akajenga Imani kwamba hata yeye anaweza akaponywa. Hakuishia hapo tu akaamua kuchukua hatua ya kupiga kelele hata uponyaji wake ukamfikia. Embu jiulize endapo angesema hayo ni maneno tu yalikuwepo tangu zamani, kina Eliya walipokuwepo.

Kama na wewe utaamua kuwa kama kipofu huyo aliesikia habari za mtu anaeponya kisha akachukua hatua na akapokea uponyaji wake na wewe pia unaweza kupokea uponyaji wa fikra zako. Muhimu ni wewe kukubaliana kwamba una upofu wa fikra na uanze kuita uponyaji wako. Hakuna mtu atakuja akulazimishe utoke nje ukaponywe, hakuna mtu atakulazimisha uende kwenye semina, hakuna mtu atakulazimisha usome vitabu. Hakuna mtu amekulazimisha pia usome Makala hii, ni wewe binafsi unaamua kuchukua hatua baada ya kutambua ule udhaifu ulionao.

Chukua hatu leo ili usibaki kama ulivyo. Njia pekee ya wewe kutokubaki kama ulivyo ni kukubali kuwa una udhaifu na unatakiwa kupokea uponyaji.

Nikutakie kila la Kheri.

Rafiki Yako Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

7 Responses

  1. Asante Sana br! Yaani Kama vile ulikuwepo kwenye ndoto yangu ya Jana! Niliota Kama ulivyoeleza juu ya kubadilisha mawazo na fikra ndipo utakapofanikiwa, MUNGU na azid kukubariki na kutimiza kusud lake kupitia wew

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading