Kwenye maisha tuna watu wa aina mbalimbali na wenye tabia tofauti tofauti. Ukiweza kukaa na watu unaweza kujifunza mambo mengi sana kwenye maisha wanayoyaishi.
Nimekutana na watu wa aina nyingi sana na wenye tabia tofauti. Tabia moja ambayo leo tutaizungumzia ni hii ya baadhi ya watu kuona kwamba wao peke yao ndio wanastahili kupata vitu fulani kutoka kwa wengine lakini wanajisahau kwamba na wao wanatakiwa watoe vitu kwa wengine pia.
Ukitaka kuonyeshwa upendo onyesha upendo.
Ukitaka kupewa vitu wape watu vitu.
Usiojione wewe ndio unastahili peke yako kusaidiwa kumbuka hata na wewe unayo nafasi na jukumu la kuwasaidia wengine pia.
Kabla hujaanza kulaumu mtu hajakufanyia kitu fulani jiangalie wewe kwanza umechangiaje kutofanyiwa kile kitu.
Ukitaka kupigiwa simu mara kwa mara wapigie watu simu mara kwa mara.
Chochote kile unachokitaka kufanyiwa na wengine anza wewe kuwafanyia wengine.
Ni kama ilivyo kanuni ya utoaji. Ukitoa utapokea.  Na usitegemee kupokea pale pale unapotoa.
Fanya mambo yote mema lakini usifanye kwa sababu unataka ufanyiwe fanya kwa sababu ndio maisha uliyoamua kuishi yaani hata kama hakuna anaekupenda wewe uendelee kuwapenda wengine.
Maana yangu kuu ni kwamba kama unahisi wewe hupendwi jaribu kuona kuna wenzako kama wewe wanaona hawapendwi ni nani atakaewaonyesha upendo?
 Anza wewe kuwaonyesha wengine upendo bila kutegemea chochote kutoka kwao.
Tendea wengine mema bila kutegemea chochote kutoka kwao.
Asante sana
Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading