Wasamehe.

jacobmushi
2 Min Read
Wako wengi sana waliokuumiza moyo katika safari yako na inawezekana uliumizwa sana na hata kusema hutasamehe. Leo ni nafasi ya kwako kuondoa yote ndani ya moyo wako ili uwe huru uweze kuondoka ukiwa salama.
Inawezekana wanakwambia kwamba hutaweza unachokifanya wamefanya wengi wakashindwa. Dawa sio kufanya ili uje kuwaonyesha kwamba unaweza au kuacha na kukata tamaa. Jawabu sahihi la kuwapa ni kuwasamehe wasamehe kwakua hawajui kwamba kila binadamu ni wa pekee hivyo kwa kushindwa kwa Fulani hakumaanishi na wewe utashindwa.
Wapo waliokwambia kwamba wewe ni mdogo sana hivyo usubiri. Huna haja ya kubishana nao kuwaonyesha jinsi gani unaweza wasamehe na endelea mbele kuzifuata ndoto zako. Kwani unajua siku yako ya kufa? Unasubiri hadi uwe na umri Fulani ambao watu ndio watakuelewa ukizungumza? Una uhakika wa kufikia umri huo? Kama nafasi ya kufanya sasa hivi ipo tafadhali fanya bila kuogopa watu wanakuonaje wewe kutokana na umbo lako dogo au umri wako mdogo.
Wasamehe wanaokudharau na kukuona unapoteza muda tu wakati wewe unajua unachokipanda sasa hivi. Wasamehe wote wanaokucheka wanaosema ukatafute kazi ya uhakika inayolipa wakati wewe umeshaamua kuanza kuishi ndoto yako hadi itokee katika uhalisia. Wasamehe wote ambao hawakuelewi vizuri unachomaanisha unapowaambia kule unakotaka kufika.
Hakuna mtu mwingine anaejua unachokitaka kama wewe mwenyewe unavyofahamu. Hakuna mtu mwingine anatakiwa afahamu unapokwenda Zaidi ya wewe unavyofahamu. Hakikisha unafahamu vyema kule unapokwenda kwani ndio mwanzo wa wewe kua na ujasiri wa kutosha na kuweza kuzishinda changamoto na kudharaulika pale unapowaeleza kile unachokitaka.

Isamehe jana, samehe makosa uliyoyafanya huko nyuma, kuna siku waliokuacha njiani wakidhani umepotea watakuja kukuona ukiwa juu kama tai. Ndipo hapo watasema aisee! Kumbe ilikua kweli yale aliyokua anayasema!
Karibu sana! Jiandae kujipatia kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai leo.
Kingdom of Success.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mhamasishaji na Mjasiriamali.
Simu +255654726668

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading