Warren Buffett — ‘The most important thing to do if you find yourself in a hole is to stop digging.’

Kitu cha Mhuhimu sana cha kufanya pale unapojikuta kwenye shimo ni kuacha kuchimba.

Shimo lako linaweza kuwa ni madeni, mahusiano mabovu, marafiki wabaya, na Maisha yasiyo na mwelekeo.

Ukijikuta wewe ni mlevi dawa ni kuacha kunywa pombe la sivyo unazidi kupotea.

Ukijikuta upo kwenye mahusiano mabovu yanayokupeleka chini dawa ni kutoka kwenye shimo.

Soma: Tabia za Watu Wenye Mafanikio

Kama una madeni dawa sio kuendelea kukopa, kuendelea kukopa ni kuendelea kuchimba shimo. Anza mpango wa kupanda kwenye shimo haijalishi ni refu kiasi gani.

Watu wengi tuna mashimo mengi kwenye Maisha yetu na yanasababisha tusionekane kwa vile tunavyovifanya. Bahati mbaya sana mashimo haya tumeyachimba wenyewe.

MUHIMU:

Leo tafuta muda uangalie upo kwenye mashimo ya aina gani? Je umekuwa unaendelea kuchimba au umeanza mpango wa kutoka na kuyafukia? Mashimo tunayo mengi na ndio sababu unakutana unafanya jambo halionekani kumbe kuna shimo upo ndani yake.

Inawezekana unajitahidi sana kazi zako zionekane lakini kumbe upo ndani ya shimo. Ukiwa ndani ya shimo ukipiga kelele ni ngumu kusikika.

Kuendelea kutengeneza chuki na visasi ni mashimo unajichimbia. Kuendeleza tabia zako mbovu ni mashimo unajichimbia mwenyewe. Tabia yeyote mbaya uliyonayo ni shimo hilo na ukiendelea kuifanya ni kuendelea kuchimba shimo. Kadiri unavyochimba shimo ndio unajitengenezea namna rahisi ya kujifukia mwenyewe.

TOKA KWENYE SHIMO.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading