Home » HATUA ZA MAFANIKIO » HATUA YA 232: Fanya Kila Siku.

HATUA YA 232: Fanya Kila Siku.

Chagua kitu ambacho utakifanya kila siku hadi kikutoe. Chagua vitu ambavyo utavifanyia kazi kila siku hadi uwe bora. Ni kwambie ukweli kama siku inapita na hakuna kitu ulichokifanya kinachoelekea kule unakotaka kwenda basi umeipoteza siku yako. Umepoteza pesa nyingi sana ambazo ulipaswa kuzipata miaka michache ijayo.

Andika kwenye NoteBook yako ni sehemu gani wewe uko vizuri Zaidi kuliko sehemu nyingine na uifanyie kazi hiyo sehemu ili kukuza Zaidi kile kilichopo ndani yako. Ukweli huwezi kuwa wa kawaida kama kila siku kuna kitu unafanya kinachoongeza thamani ya kile kilichopo ndani yako.

Huwezi kuwa wa kawaida kama kila siku kuna kitu unafanya kiachoongeza thamani yako.

Huwezi kubakia palepale ulipo kama kila siku kuna hatua unapiga.

Huwezi kukosa kitu cha kufanya kama utakuwa unajilazimisha kufanya hata kama hautaki. Jitengenezee nidhamu ya kufanya kile ulichoamua bila ya kujali upo kwenye hali gani.

Usikubali kupoteza muda wako kwa vitu ambavyo haviongezi thamani yako hasa kwa upande ule ulioufanyia kazi.

Itakuwa ni vichekesho unataka kuwa mwalimu mzuri halafu muda mwingi upo kwenye Tv unafuatilia yaliyojiri kuliko unavyokaa na vitabu.

Itakuwa ni ajabu sana kama wewe unataka kuwa tajiri halafu hakuna cha maana unachokifanya kwenye maisha yako kianchoelezea unapokwenda.

Kuna msemo unasema ukitaka kujua mtu anakwenda wapi usisikilize maneno yake angalia matendo yake. Matendo yako yanaelezea kwa wazi Zaidi kule unapokwenda kuliko unavyoongea.

Vipaumbele vyako vya kila siku vinaonyesha kule unapokwenda. Kama vipaumbele vyako havna hata tukio moja linalopelekea kuitimiza ndoto yako unapoteza muda rafiki.

Fanya kila siku.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

About

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: