Kujua kile unachokitaka ni jambo la kwanza, kinachofuata ni kufahamu gharama ambazo unapaswa kulipa ili kufika pale unapotaka. Wengi wanaishia kwenye kujua wanachotaka na kukata tamaa baada ya kuambiwa gharama wanazotakiwa kulipa.

 

Ni vyema ukajiuliza maswali haya na ukapata majibu yake wakati unaanza safari yako.

Unajua gharama gani unapaswa kulipa ili ufike unakotaka kwenda?

Upo tayari kulipa gharama?

Upo tayari kujitofautisha na wengine?

Upo tayari kuvumilia changamoto utakazokutana nazo baada ya kuanza safari ya kulipa gharama?

Tuna watu wengi ambao hua wanaishia hapa mar azote na wakati mwingine wanashindwa kufanya chochote ambacho kingeweza kuonyesha nia yao ya kweli kwenye yale wasemayo wantaka.

Huwezi kuepuka kulipa gharama, ili uweze kutoka lazima ukubali kulipa gharama.

 

Kama ni kujifunza, kutengeneza mtandao wa watu ambao wanakuamini. Kujenga watu ambao wataweza kwenda na wewe.

Kulipa gharama ndio kunaonyesha ni kiasi gani umejitoa kwenye kile unachokifanya. Wengi hawataki kulipa gharama lakini wanataka matokeo.

Kwenye kulipa gharama kuna maumivu utayapata wakati mwingine. Kwenye kulipa gharama kuna hatua utapaswa kuchukua za ziada.

Usikubali kuishia hewani nenda mbele Zaidi ili uweze kuutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako.

 

Kitu ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba bado hujachelewa bado una nafasi ya kufanya makubwa hata yale ambayo umekuwa unasitsita kila wakati bado nafasi ipo na ndio maana upo hai leo.

Amua sasa kufanya chukua hatua sasa usiishie njiani na maisha yako yatabadilika.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading