HATUA YA 269: Huhitaji Kikubwa Sana.

jacobmushi
2 Min Read

Mara nyingi tunafikiri ili ufikie hatua kubwa kwenye maisha lazima uanze na mwanzo ambao ni mkubwa sana. Usifikiri kwamba ukiwa na vitu Fulani na Fulani basi ndio maisha yako yatakwenda vizuri.

Kama umeshindwa kutumia rasilimali ulizonazo sasa hivi hata ukipewa kubwa bado utashindwa na unaweza ukaharibu badala ya kutengeneza.

Uwezo wako unapimwa kwa namna ambavyo umeweza kutumia rasilimali zile chache zilizokuzunguka. Mwaka 2014 ilikuwa ni mwaka ambao nilianza safari hii ya kuandika nikiwa na msukumo mkubwa kutoka ndani yangu na sio ukubwa wa vitu vilivyokuwa vimenizunguka.

Badala ya kubakia chini na kujiiona huwezi kujiona huna kitu Fulani amua kuchukua  na hatua fanya maamuzi ili uweze kufikia kile unachokitamani. Hakuna aliewahi kupata alichokuwa anakitaka kwa kuendelea kulalamika.

Hakuna aliewahi kupata alichokuwa anakitaka kwa kuendelea kulaumu hali na mazingira aliyonayo. Haijalishi watu wamekuangusha kwa kiasi gani kikubwa ni namna ambavyo wewe umeamua kuchukua hatua kutoka hapo ulipo.

 

Maisha ya wengi yataguswa kwa wewe kuamua leo kuchukua hatua. Kuna wengi wanatakiwa wajifunze kupitia wewe lakini hawawezi kwasababu mpaka sasa hakuna ulichofanya Zaidi ya kutoa sababu kila siku.

Chukua hatua hata kama ni kidogo lakini kuwa kuna thamani inatengenezwa kila siku. Sio lazima uwe na mwanzo mkubwa ndio utaweza kutefikia unakotaka kwenda.

Kwenye kitabu cha biblia kinasema unapokuwa na Imani kama chembe ya haradali unaweza kuhamisha milima. Hii ikiwa na maana haijalishi mbegu iliyoko ndani yako ni ndogo kiasi gani bado inaweza kufanya makubwa kama itapandwa sehemu ambayo ina udongo mzuri pamoja na kuhudumia.

Ukubwa sio chochote bali Imani yako ndio inatakiwa iwe kubwa. Kama utaanza na vikubwa huku una Imani ndogo, una hofu na mashaka utaishia kupata hasara.

Imani yako juu ya mafanikio inatakiwa iwe na nguvu kuliko kile ambacho unakiogopa.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading