Mojawapo ya sifa kubwa ambayo inamtofautisha mwanadamu na viumbe wengine ni kufikiri. Na sio kufikiri tu na baada ya kufikiri kufanya maamuzi ambayo yatamwezesha aendelee kuishi. Ili uweze kufikiri sawasawa ni muhimu sana kama binadamu uwe na tabia ya kuweza kujifunza ili usiwe kama viumbe wengine ambao uwezo wao wa kufikiri siku zote unafanana.
Mtu yeyote anaedhani yeye anajua kila kitu ni mojawapo ya watu wasiojua chochote kabisa. Kwa kawaida kama huwezi kujua ni muda gani usingizi ulikuchukua ukalala basi ni ukweli kwamba kuna vitu vingi sana huvijui.
Mhitimu ambaye namzungumia ni mtu yule ambae hujiona yuko sawa kwenye kila jambo ambalo analifanya. Binadamu ambaye yeye hata kabisa kuonekana amekosea kwenye chochote anachokifanya sio binadamu wa kuambatana nae.
Kama unataka kufika mbali kwenye lolote ufanyalo waepuke watu wanaojihesabia haki kwenye Maisha yao. Waogope watu wanaoogopa kukosea au kuonekana wamekosea.
Unatakiwa ukubali kujifunza kwa kila mtu anaekuja kwenye Maisha yako. Unatakiwa uwe ni mtu ambaye unapenda kuambiwa makossa yako na sio mtu wa kukasirika pale unapoambiwa hapa umekosea.
Hivi unajua hata Mungu kuna vitu anajifunza kwenye Maisha ya wanadamu? Kuna namna tunaishi yeye akitutazama anatushangaa na kujifunza vitu. Sina uhakika na hilo lakini kutokana na mambo ambayo yanafanyika kwenye ulimwengu wa sasa lazima kuna vitu ambavyo Mungu anasema Looh!
Soma: NILICHOJIFUNZA KWENYE MAISHA YA WENGINE
Kinachoshangaza ni kwamba kuna watu hawataki kujifunza wanaojiona wao wameshajua kila kitu. Unapaswa kutambua kila iitwapo leo kuna kitu kipya cha kujifunza ili uweze kuendelea kuwa na siku nyingine bora Zaidi.
Nguvu yako kubwa ipo kwenye ufahamu wako kama utauzuia ufahamu wako kujifunza basi ni kwamba utakuwa unajinyima nguvu Zaidi ambazo zipo ndani yako. Kila changamoto unayopitia ina somo ndani yake, kila mtu anaekusumbua ana somo unapaswa kujifunza.
Usikubali kuishi Maisha sawa na Wanyama wengine wewe una uwezo mkubwa kama utakubali kujifunza kila siku na kwenye kila hali hapa duniani. Huwezi kuwabadilisha watu bali unaweza kujifunza namna ya kuishi nao.
”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com