Katika mambo ambayo kila mwanadamu ana uhakika kwamba lazima yatokee kwenye Maisha yake mojawapo ni kifo. Kila mmoja anajua kwamba ipo siku ataondoka duniani, japokuwa hakuna ajuae ataondoka siku gani na kwa njia ipi.

Kinachoshangaza sana ni watu ambao wanakuwa na hofu sana wakiwaza juu ya kifo au siku ya kufa kwao. Hii inatokana na watu wengi kutokutambua kwanini wapo hapa duniani. Unajua lazima kifo kikutishe kwasababu hicho unachokifanya sasa hivi sio kile ambacho ulizaliwa kuja kukifanya hapa duniani.

Kama utaweza kulijua kusudi la kuumbwa kwako na ukaanza kuliishi hupaswi hata kidogo kuogopa kuhusu kifo. Hii ni kwasababu kusudi lako lazima litimie kwanza ndipo uweze kuondoka hapa duniani. Hatuwezi kusema lini litatimia ila yeye awezaye yote ndie ajuae.

“Stop whatever you’re doing for a moment and ask yourself: Am I afraid of death because I won’t be able to do this anymore?”

― Marcus Aurelius, Meditations

Mwanafalsafa Marcus anasema acha mara moja kile unachokifanya kwa muda kisha ujiulize; naogopa kifo kwasababu nikifa sitaweza kuendelea kufanya hiki ninachokifanya sasa hivi? Swali hili ni la muhimu sana kwako Rafiki yangu hasa juu ya kile unachokifanya.

Kama kweli unaliishi kusudi lako basi kifo kitakutia huzuni kwamba siku ukifa hutaweza tena kuimba, kuandika, kufundisha, kuzungumza na watu, kugundua vitu mbalimbali. Na mengine mengi ambayo Mungu ameweka ndani yako. Ukianza kuona huhamasiki kufanya Zaidi unachokifanya pale unapokumbuka kifo basi ujue hilo sio kusudi la wewe kuwepo hapa duniani.

Kama ukiwaza kifo chako hupati nguvu mpya ya kuendelea kufanya kile unachokifanya basi jiulize mara mbili mbili kama ni kweli ulizaliwa kuja kufanya jambo hilo. Kifo kinatakiwa kiwe hamasa kwetu ili tufanye Zaidi, tutoe vyote vilivyopo ndani yetu tuviache hapa duniani.

Kifo hakitakiwi kuwa huzuni kwetu bali hamasa ya kufanya Zaidi na Zaidi yale ambayo Mungu ametuumbia kufanya. Ukishaona ukiwaza kifo unasema “najitesa ya nini wakati nitaviacha vyote” ujue bado hujajitambua sawa sawa. Kama umebarikiwa uwezo wa kutafuta hela zitafute sana, anzisha makampuni makubwa. Yote hayo sio kwa ajili yako wewe bali ni kwa ajili ya kutimiza kusudi la Mungu.

Acha Alama.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading