#HEKIMA YA LEO: Kubali kufundishwa

Ukijifanya unajua, unakuwa mpumbavu. Maana kujifunza ni kama pumzi ukishavuta lazima utoe iliyochafuka kisha uvute tena.

Ukikubali kuwa mwanafunzi ndio utaona sehemu nyingi ulizokuwa unakosea. Pia Utagundua kwamba bado kuna mambo mengi hujui.

Ukikubali kufundishwa unatakiwa ukubali pia kukosolewa. Unapokuwa na Mwalimu wako akakwambia hapo umefanya vibaya kubali usichukie ili uweze kujifunza zaidi.

Wanadamu tunapenda kupewa sifa na kuambiwa tumefanya vizuri. Lakini tunapoambiwa tumekosea tunajisikia vibaya. Unapokuwa mwanafunzi kubali kukosolewa na Mwalimu wako.

Duniani kuna mengi ya kujifunza kwa watu kama utakubali kuwa myenyekevu na msikilizaji mzuri. Kila mtu ana kitu ambacho anakijua wewe hukijui haijalishi ni nani. Kubali kujifunza kwa wengine bila kujali umewazidi kitu gani.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading