#HEKIMA YA LEO: Vidogo Vyenye Manufaa..

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.

MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Kwenye mtihani shuleni tulikuwa tunaambiwa yale maswali ambayo unayaweza ndio unatakiwa uyafanye mapema sana kabla akili haijachoka, yale magumu ndio utayafanya baada ya kumaliza yale ambayo una uhakika nayo.

Ukitumia nguvu nyingi kwenye yale ambayo uwezo wako ni mdogo unakuwa unajipa nafasi ya kukata tamaa mapema na hata kushindwa kufanya yale ambayo una uwezo wa kufanya.

Daudi alipomwona Goliathi hakuangalia sehemu nyingi alizojiziba na chuma kwa haraka haraka macho yake yalimpeleka kwenye paji la uso lililokuwa wazi hivyo na yeye akalenga palepale.

Walikuwepo mafundi wa kurusha mishale pale vitani lakini hakuna alietazama paji la uso lililokuwa wazi wote walikuwa wanatazama yale manguo ya chuma aliyovaa. Wote walitazama kifuani palipojaa chuma wakasahau kwamba mshale ungeweza pia kupita kwenye paji la uso.

Wewe tatizo lako unatazama mambo makubwa kumbe ili uweze kutimiza haya makubwa ungefanya jambo moja dogo tu ambalo ulikuwa unalidharau au kuliona halina matokeo makubwa.

Yale mambo magumu kwenye Maisha yako ambayo huwezi kuyabadili nikiwa na maana kwamba yapo nje ya uwezo wako kwa wakati huo, inakupasa ukubali ukweli huo kisha usonge mbele katika kutazama kile ambacho una uwezo nacho.

Tafuta kidogo chenye manufaa, endelea kutafakari ni wapi ambapo ukisema uchukue Hatua utakuwa ndio mwanzo wa wewe kuelekea kufanya yale makubwa unayoyataka.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

https://jacobmushi.com/patavitabu/

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading