Tag Archives: chukua hatua

537; Ingia Ndani Zaidi..

Watanzania wengi ni wavivu sana kusoma, kabla hujaamini picha ya kichwa cha habari inayosambazwa jaribu kutafuta habari nzima uisome na uelewe. Vichwa vingi vya habari huandikwa kwa namna ya kuvuta wasomaji na bahati mbaya sana wengi wenu huishia kusoma kichwa tu na kufikia hitimisho. Usiwe mwepesi pia kuamini kila kilichoandikwa kwasababu kwenye ulimwengu wa sasa… Read More »

HATUA YA 342: Unaemngoja Anakungoja Wewe.

Inawezekana kuna mtu unamngoja aje afanye jambo kwenye Maisha yako ili yabadilike. Inawezekana kwenye akili yako unasubiri ipo siku mambo yatakaa sawa na kuwa marahisi Zaidi ya sasa. Inawezekana pia kuna muujiza Fulani unautegemea kwenye akili yako utokee ndio kila kitu kibadilike kwenye Maisha yako. Napenda kukwambia Rafiki huyo unaemngoja afanye yote hayo anakusubiri wewe… Read More »

#HEKIMA YA LEO: Vidogo Vyenye Manufaa..

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote. “NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA. MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.” Kwenye mtihani shuleni tulikuwa tunaambiwa yale maswali ambayo unayaweza ndio unatakiwa… Read More »

#HEKIMA YA JIONI: Kuchukua Hatua.

Hatuhitaji watu wengi wanaoweza kulielezea jambo Fulani vizuri bali tunahitaji watu wachache wanaoweza kuchukua Hatua juu ya jambo husika. Tuna upungufu wa watu wanaochukua Hatua ndio maana hatuna maendeleo.   Badala ya kuendelea kuongea maneno matupu fanya kile kilichopo kwenye uwezo wako kwanza. Kwa kupitia hicho ndio utaona uwezekano wa kufanya makubwa Zaidi. Tuna wengi… Read More »

KONA YA BIASHARA: Yajue Mapungufu Yako.

Ni vyema kwa kila mmoja akaweza kutambua ni wapi ana mapungufu na kuyafanyia kazi kabla hayajaleta madhara kwenye kazi. Kila binadamu ana mapungufu yake ndio maana haupo mwenyewe huku duniani. Kuna sehemu unateleza na yupo mtu ataweza kuwa msaada wako. Unapoyajua mapungufu yako unajipa nafasi ya ushindi mzuri kwenye biashara yako. Ukae ukijua kwamba mapungufu… Read More »

USITAZAME LEO

Leo vita ni vingi sana, Leo hakuna mavuno bado. Leo wanakusema wengi Leo inaonekana kama ni ngumu sana. Leo inaonekana kama utakwenda kushindwa. Leo inakatisha tamaa sana. Leo unatoka jasho jingi sana. Leo unatumia nguvu nyingi sana.   Ukitazama leo utakata tamaa Ukitazama leo utarudi nyuma. Ukitazama leo utayaona magumu. Itazame ndoto yako. Yatazame mazao… Read More »

#USIISHIE_NJIANI: Kuna cha Kujifunza?

Kwa lolote lile ambalo unapitia kwenye maisha yako sasa hivi. Liwe zuri au liwe baya ni vyema kuwa na muda wa kujiuliza swali kwa yote hayo unayopitia ni yapi unajifunza? Kwa yote yanayoendelea kwenye maisha yako ni somo gani unaondoka nalo? Usikubali tu kuishia kuumia au kufurahi bila kuondoka na somo lolote. Ukiwa mtu ambaye… Read More »

#USIISHIE_NJIANI: Hali Mbaya Uliyonayo Inasababishwa na Hiki

Leo jioni nikiwa nazishika ndevu zangu ghafla katika fikra yakanijia maneno ambayo niliambiwa miaka karibia kumi iliyopita. Kuna mtu mmoja aliniambia “wewe ukiwa na ndevu utakuwa mbaya sana”. Nikabaki najiuliza kwanini haya maneno yamekuja sasa hivi wakati nashika ndevu? Mbona ni muda mrefu sana umepita na nilishayasahau kabisa? Nikagundua kwamba maneno uliyonenewa na watu yanabaki… Read More »

#USIISHIE_NJIANI-  Jawabu la Unachokitaka ni Hili hapa.

Penda kujipa muda wa kusubiri matokeo unayoyataka wakati unayafanyia kazi. Bahati mbaya hatuna kipimo maalumu cha muda ili uwe na uhakika wa unachokisubiria. Kama mwanamke amebeba ujauzito inafahamika kabisa ni baada ya miezi tisa atajifungua. Na endapo itatokea tofauti na hapo muda ukizidi tunaanza kupata wasiwasi. Kwenye mafanikio hakuna mahesabu ambayo yapo na uhakika kabisa… Read More »