524; HEKIMA: Panda Mti

jacobmushi
4 Min Read

Katika kutafakari sana siku ya leo juu ya Maisha yetu hapa duniani, nimekutana na jambo hili la ajabu sana. Nasikia kabisa Mungu anasema nikwambie, nizungumze na wewe ambaye umekata tamaa katika sehemu mbalimbali za Maisha yako.

Unajua unaweza kufanya vitu vya aina mbalimbali vyote vikaharibika bila kukuletea mafanikio yoyote. Njia rahisi unaweza kuchagua ni kukata tamaa na kujiona wewe huwezi chochote. Sasa leo nataka ukafanye jambo hili la muhimu sana kwenye Maisha yako na dunia kwa ujumla.

Umefikia mahali unaona wewe hujawahi weza kukaa kwenye mahusiano yakadumua hata siku moja. Nenda Katafute mti unaoupenda sana Uoteshe (Panda Mti)

Umefikia mahali unaona kila biashara unayofanya unafeli yaani hujawahi kabisa kupata mafanikio kila ukijaribu unashindwa.

Otesha Mti.

Umejaribu njia mbalimbali kutafuta mtoto na hadi sasa hujapata.

Otesha Mti.

Umefikia Hatua unataka kujiua kwasababu unaona hakuna anaekupenda.

Nenda Kapande mti unaoupenda uwe unauhudumia.

Watu wanasema wewe hutaolewa tena umri umeenda.

Nenda Kaoteshe Mti.

Kila unachokifanya kinaharibika.

Otesha Mti.

Unajiona wewe hakuna cha maana ulichofanya hapa duniani.

Otesha Mti.

Ndio inawezekana kuna mengi unapitia kwenye Maisha na umefikia mahali unasema sasa mimi nimechoka kabisa.

Katafute tunda la mti unaoupenda uoteshe uanze kuuhudumia.

Kama hujaweza hata kufanya chochote cha maana kule kwenu na unaona aibu hata kurudi nyumbani.

Tafuta muda nenda Otesha mti wa matunda na uwaambie wauhudumie na kuupenda kama ambavyo wangekufanyia wewe.

Kuna mtu ulimpenda sana na imeshindikana kuwa nae. Nenda kaoteshe mti uutunze na kuuhudumia vizuri kama vile ambavyo ungefanya kwa yule uliekuwa unampenda.

Umempoteza mpenzi wa Moyo wako kwa kifo (Pole Sana). Nenda kaoteshe Mti.

Miaka 10 ijayo mti huu uliootesha leo utakufundisha kitu kikubwa sana kwenye Maisha yako kama bado utakuwa hai. Kama hautakuwepo hai basi utakuwa ni alama kubwa kwa wale uliowaachia.

Embu jiulize ukijiua sasa hivi kwasababu Maisha ni magumu au ukatoroka na kutelekeza familia utakuwa umeacha alama ya aina gani?

Ukiotesha mti ambao unaweza kuupata bure au kununua mche kwa gharama ndogo sana mti huo unaweza kuja kuwa alama kubwa sana kwa wale unaowapenda.

Ipo siku watakula matunda ya mti huo na watakukumbuka. Ipo siku watakaa kwenye kivuli cha mti huo na watakukumbuka.

Usiseme wewe huwezi kitu bado una kitu unaweza kufanya na kikaacha alama hapa duniani. Usiojione wewe kila unachokifanya basi hakiwezekani naamini ukiotesha mti utaota. Ukiotesha mti utaweza kuuhudumia hadi ukakua.

Sasa Rafiki yangu wewe ambaye kuna kitu umekuwa unakitafuta kwa muda mrefu bila ya mafanikio hapa duniani naombe ukaoteshe mti. Mti huu uwe ni alama kwa niaba ya kile ulichokuwa unakitafuta. Endapo utapata ulichokuwa unakitafuta mti huu utakufundisha uvumilivu, endapo utakikosa basi mti huu utakuwa umeacha alama kwa kile ulichokuwa unakitafuta.

Usikubali kusema huwezi, unaweza kuotesha mti na mti huo ukawa alama kubwa sana hapa duniani.

Kupata huduma na Bidhaa mbalimbali kwenye mtandao huu bonyeza linki hii www.jacobmushi.com/kocha

Makala hii imeandikwa na Kocha Jacob Mushi. Mwandishi wa Vitabu na Makala, Kocha wa Maisha, na Mjasiriamali.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
2 Comments

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading