Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.
Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.
“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”
Pamoja na kwamba wengi tumekuwa na maono makubwa na ndoto kubwa kuna mengi sana ambayo tunakutana nayo kila siku yanaweza kuwa sababu ya kutupunguzia mwendo wetu au kusimamisha kabisa. Mfano ukiwa na marafiki ambao hawana Ndoto kubwa na unatumia muda mwingi Zaidi kuwa nao watakuambukiza. Ni vyema ujue je hapo ulipo sasa hivi ndipo ulitakiwa kuwa?
Umeridhika na Hapo Ulipo?
Kama umeanza kuona matokeo unayopata yanatosha yaani kuna kauvivu Fulani hivi kameanza kukujia pale unapofikiria kujituma Zaidi ujue umeshaanza kuhama njia. Kama huwazi tena kupanuka Zaidi yah apo ulipo, kama ni biashara huna mpango wa kuongeza wateja wapya ujue umeshapotea kwenye mstari.
Tabia zinaweza kuwa ndogo ndogo usizijue lakini kumbe ndio zimeshakuathiri na zinakufanya uendelee kubaki hapo. Utakuja kugundua tu ile siku mambo yatakapokuwa mabaya.
Umeacha Kufanya Yale Ya Msingi.
Kuna yale mambo ya msingi sana ambayo tunatakiwa kufanya ili tuweze kutengeneza Ndoto zetu. Mfano ni uadilifu, ukiona umeanza kuacha mambo hayo unaanza kufanya unachotaka, ujue umeshapotea.
Kama una biashara basi unakuta hujali tena wateja na wala huweki tena vile viwango vya ubora kwenye bidhaa na huduma zako. Tabia hizi ni za hatari sana na zinaleta maanguko makubwa.
Wiki Mbili zilizopita Umekuwa Unafanya Kitu Gani?
Jiangalie kwa haraka haraka, je ni mambo gani umekuwa ukiyafanya kwa wiki mbili tatu zilizopita? Kama ulokuwa unafanya hayahusiani hata kidogo kwenye kukupeleka kutimiza Ndoto zako jua ushahama njia. Inawezekana umehamia kwenye mambo ambayo yanakuwa ni kupoteza muda badala ya mambo ya msingi kwenye Maisha yako.
Jambo La Kufanya:
Jifanyie Tathmini Mara Kwa Mara.
Jenga tabia ya kufanya tathimini ya maendeleo yako kila siku, kila wiki mwezi na hata mwaka. Unapokuwa unafanya tathmini za mara kwa mara zinakuonyesha kama kweli unakoelekea ni kwenye Ndoto yako au umeshahama kwenye mstari.
Pia utafahamu kama unakua au unaporomoka.
Kaa na Watu ambao Wanakuhamasisha Kusogea Mbele.
Siku zote kaa karibu na watu ambao wanakupa hamasa ya wewe kutamani kufanya makubwa Zaidi. Watu hawa wanaweza kuwa familia yako, watu waliofanikiwa Zaidi yako, mpenzi wako na wengine wengi. Usikubali kukaa na watu ambao watakuwa wanakunyonya nguvu, watu ambao kila wakati wao wanalalamika tu.
Kama unatafuta mchumba ukaenda kijiweni kusikila hadithi unaweza ukarudi nyumbani unasema sitakaa nioe kabisa. Tafuta sehemu ambayo inakupa hamasa ya kusogea mbele na wala sio kurudi nyuma.
Acha Kufuatilia Habari Hasi.
Usipoteze muda wako kulisha akili yako habari hasi, kwanza mar azote huna uwezo wowote wa kuamua katika yale ambayo unayafuatilia. Unaishia kujaza moyo wako hasira na visasi juu ya watu wasiojulikana. Kumbe ungetumia muda huo kusomana kufanya mambo ya msingi Zaidi ungeweza kuwasaidia vizuri wengi ambao wanateseka.
Tumia muda wako vyema ili uweze kuleta mchango mzuri kwenye Ndoto zako.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog
Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/