Unafahamu pamoja na kuwajua watu wengi sana katika Maisha yako kuna watu angalau 10 tu ambao wanaweza kuwa tayari kukuinua pale unapokuwa umeanguka chini? Mtu wa kawaida kabisa ana watu wake wa karibu 10 ambao wapo tayari kununua au kuchangia kila anachokifanya. Ukweli ni kwamba hawa kumi wanaweza wasitoshe kununua bidhaa yako au kulipia huduma yako na Maisha yako yaende kama ambavyo unataka.

Hawa kumi ni wale ambao huhitaji kutumia nguvu nyingi kuwaambia au kuwatangazia ndipo wanunue kile ulichotoa. Ukitaka kujua hili ni kweli anza biashara yeyote leo kisha watumie ujumbe watu mia moja walipo kwenye simu yako uone ni wangapi watajibu na kukwambia uwaletee hiyo bidhaa. Kuna wengine hawatakujibu kabisa, lakini kuna watu kama kumi hivi ambao watakuwa chanya na watasema uwaletee hiyo bidhaa.

Soma kitabu; MBINU 101 ZA MAFANIKIO

Kanuni hii ya 10× ameanzisha Mwandishi wa Vitabu anaejulikana kwa jina la Grant Cardone, ambapo amendika na kitabu chake kabisa kiitwacho 10× Rule. Sitakwenda kukichambua kitabu ila nitakuelezea tu namna ambavyo utaweza kuitumia kanuni hii kwenye chochote kile ambacho unataka kuanzisha na kinawahusu watu.

Hawa watu kumi ambao wapo tayari kukupa sapoti yao kwa namna yeyote ile unaweza kuwatumia Zaidi ya kuwauzia bidhaa peke yake. Ndio maana linakuja neon la 10× yaani 10 mara, sasa inaweza kuwa 10×5, 10×10, 10×100, au vyovyote vile ambavyo wewe unavyoweza kuamua kuweka hapo. Tukichukulia mfano rahisi kabisa ni kwamba hao watu kumi wanakupa sapoti ya nguvu wanawajua pia watu kumi nyuma yao. Yaani kwa mahesabu ya haraka haraka jumla yao watakuwa na watu 100.

Kama utaweza kuwatumia vizuri hawa watu kumi ukahakikisha wamependa bidhaa yako na wakaikubali yaani ukatengeneza bidhaa bora kiasi kwamba watu wakaikubali na wakawa hawana wasiwasi hata kidogo juu ya bidhaa hiyo. Unaweza kuwaambia wakawashirikishe na marafiki zao wanaowajua. Sasa hao watu kumi katika kuwashirikisha marafiki zao wa karibu kwa makadirio tunaweza kusema watapata kila mmoja watu 10 ambao wanaaminiana tena. Hivyo inakuja jumla ya watu 100.

Kama ni biashara ulianzisha basi hapo unakuwa umeweza kupata wateja 100. Lakini ukumbuke kwamba hili halitokei kwa siku moja au mwezi mmoja peke yake. Inaweza kuchukua hata miezi sita. Hii inaweza kutokana na aina ya biashara unayoifanya au watu pia wanaweza kuwa wazito kukuamini.

Nguvu kubwa unapaswa kuiwekeza katika wale watu kumi wa mwanzo. Hakikisha unawahudumia vizuri sana kiasi kwamba hawapati wasiwasi na wewe hata kidogo. Kiasi kwamba wakikufikiria wewe wanawaza juu mambo mazuri ambayo umewafanyia.

Ukiweza kuwahudumia vizuri utajikuta kwamba hujawaeleza  chochote lakini utashangaa wanawaleta marafiki zao kwenye biashara yako. Sasa wewe usikimbilie kuwaambia wawalete Rafiki zao kama bado hujahakikisha wamekubali na kuamini kabisa kile unachokifanya na sio wananunua kwasababu ya urafiki wenu na ukaribu tu.

Ukiweza kutengeneza watu 100 ambao wanakuamini na kukubali kwa kiwango cha juu Rafiki yangu wewe unakwenda Hatua nyingine ya mbali Zaidi sana. Unajua hesabu yako inakujaje hapo? Yaani inakuwa ni 10×100 yaani hapo jibu linakuja 1000 yaani elfu moja. Watu mia moja wakienda kuwaleza watu 10 wa karibu yao kuhusu huduma nzuri ambayo wamepata kwako moja kwa moja unaweza kutengeneza wateja jumla elfu moja.

Unaweza kuona kama huu mchezo ni mrahisi sana eeh, yaani unazidisha namba tu zinakuja wateja elfu moja. Yaani unawaambia tu wanaenda kuwaambia na wanakuja elfu moja? Hapa Rafiki hapo itakupasa ukubali kufanya hicho ukifanyacho kwa muda mrefu sana. Itakupasa uweke nguvu kubwa sana kwa miaka kuanzia 3 hadi 10. Sio kitu cha mwaka mmoja.

SOMA: MAFANIKIO KWENYE BIASHARA

Kama wewe ulijua nakwambia kitu cha kufanya kwa miezi mitatu hivi basi utakuwa umepotea. Lazima ukubali kuwa mvumilivu. Inawezekana ikatokea mapema Zaidi ya miaka mitano kutokana na aina ya kile unachokifanya. Pia inawezekana ukapata nguvu kubwa kutoka kwa watu ambao watakuja kukusaidia ukavuka haraka lakini mimi sikufundishi juu ya vitu ambavyo havitokani na nguvu yako mwenyewe. Ni kweli unaweza kufanikiwa kufikia hao elfu moja mapema Zaidi kulingana na watu ambao ulionao wewe. Na inaweza kuchukua hata miaka 5 hadi kumi kwa mtu kuweza kufikia kwenye elfu moja.

Unajua watu elfu moja wanaweza kukupa kitu gani? Tusema hao watu elfu moja wanaweza kununua bidhaa kwako ambazo kwa jumla ndani ya mwezi mmoja utaweza kutengeneza tsh elfu kumi tu kwa kila mmoja yaani kama shilingi mia tatu tu kwa siku. Ukizidisha 1000×10,000 kwa mwezi utaweza kutengeneza shilingi milioni kumi.

Hiyo elfu kumi ni mahesabu madogo sana lakini unaweza kuwa na vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kukupa faida kubwa Zaidi. Kumbuka hao watu elfu moja wkaishakuamini unaweza kutengeneza bidhaa yeyote mpya na ikanunuliwa kwa haraka sana kwasababu walishakuamini tangu zamani.

Cha muhimu wewe ni kuendelea kufanyia kazi kile ambacho unakifanya. Weka malengo makubwa ambayo yatakusukuma kila siku uchukue Hatua. Fanya kazi kwa bidi. Hakikisha hakuna mtu mwingine anaweza kukuta yaani tumia ule uwezo wako wa kipekee kwenye kile unachokifanya.

Ili uweze kuwafikia hao watu elfu moja hutakiwi kuishia Njiani.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading