Ukishakufa ubongo wako unaoza na kila kumbukumbu iliyokuwepo humo inapotea. Chochote ulichotaka kufanya kinapotea. Chochote ambacho hukukitoa nje hakitokaa kionekane tena. Dunia itakusahau kama uliwahi kuwepo. Kule unapokwenda inawezekana ukakutana na adhabu kali sana kwasababu uliondoka hapa duniani bila kufanyia kazi kile Mungu aliweka ndani yako.

Kile kilichopo ndani yako unaweza kukitoa kwa njia kuu mbili:

a/ Kufanya

Hapa utatakiwa kufanyia kazi kile kilichopo ndani yako hadi uhakikishe kimekuwa au kimeanza kuonekana. Hata kama hutakifikisha pale ulipokuwa unataka tayari utakuwa umewapa mwanga wengine na wataweza kuendeleza pale ulipoishia.

Aliegundua Taa hakutengeneza taa ya kwanza kama hizi tulizonazo leo. Aliegundua computer alitengeneza computer kubwa kama nyumba lakini watu wameyaendeleza Mawazo yake na kufikia kiwango cha juu sana.

Ni muhimu sana kuhakikisha kile Mungu ameweka ndani yako unakifanya kwasababu huo ndio mwanzo wa kutimia hata kama utaanza kwa kidogo.

Kwenye kitabu changu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO siri ya 6 nimezungumzia kuendeleza walipoishia wengine. Maana yake pale ulipoishia wewe inawezekana wakaendeleza wengine na kuyatimiza yale maono yako.

Usiishie Njiani n ahata kama ikatokea ugonjwa au kifo kimesababisha uishie njiani basi wapo watakaokuja kuendeleza pale ulipoishia.

b/ Kuandika.

Njia ya pili ya kuweza kutoa kila kilichopo ndani yako ni kuandika. Ndungu yangu kama wewe una Mawazo makubwa sana ya kupindua huu ulimwengu na umekosa namna yoyote kabisa ya kufanya basi anza leo kuchukua hatua ya kuandika Mawazo yako.

Unaweza Kuandika Kile kilichopo ndani yako kama kitabu na watu wakasoma na wakafanyia kazi Mawazo yako. Hawa wanaweza kuwa Watoto wako, ndugu zako au mtu yoyote ambaye atapendezwa na kile ulichoandika.

Andika kama kwenye kumbukumbu za aina mbalimbali. Mojawapo ya njia ambazo babu zetu walikuwa wanatumia kuwasiliana na kutunza taarifa ilikuwa ni kuandika kwenye mawe, Ngozi na sehemu mbalimbali. Sasa siku hizi teknolojia imekuwa kubwa na unaweza kuandika kwa kutumia computer, notebook yako, unaweza kuwa na blog/website ambayo utakuwa unaandika Mawazo yako na wengine tutayasoma na kuyafanyia kazi.

Kuandika sio lazima uandike mafundisho, hapa unaweza kuandika chochote kile unachoona kinafaa kusomwa na mtu na kikamsaidia.

Ule ujuzi ulionao unaweza kuutoa kwa njia ya maandishi na watu wakasoma na ukawasaidia.

Zile ndoto ulizonazo na unaweza kuziandika watu watazisoma.

Ndugu yangu usikubali hata siku ukafa na vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yako, hakuna sababu yoyote tena ya kufa na vitu. Anza sasa kuandika, watasoma Watoto wako, na wakipendezwa navyo watafanya.

KUMBUKA: Bado hatujawa na teknolojia ya kuweza kuchukua vitu vilivyopo kwenye bongo za watu hivyo basi tumia njia hizi ili utoe kile Mungu ameweka ndani yako kwenye dunia hii. Ulipewa kwa ajili ya dunia sio kwa ajili yako, usikubali kufa kabla dunia haijafaidi kile ulichokuja nacho. Itakuwa ni majuto huko utakapokwenda ukija kujiona ulikufa na suluhisho za matatizo ya mamilioni ya watu hapa duniani kwasababu tu uliamua kukaa kimya.

Ni Mimi Rafiki Yako;

Jacob Mushi

Nifuate WhatsApp: Bofya https://whatsapp.com/channel/0029Va8DmtY0LKZIjnSyEQ17

2 Responses

  1. Mkuu habari,nimeona maandiko yako nimependa napataje kitabu kilichonisisimua nimeona jina lako na mimi naitwa ivo ivo jacob mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading