#USIISHIE_NJIANI: DUNIA INAKUTAZAMA.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Wakati unaanza ulianza kwa mbwembwe na kelele nyingi, ulipenda kila mmoja ajue kwamba unaanza biashara au kipaji chako. Kuna waliokupinga, waliokukatisha tamaa, waliokutia moyo, waliosema umechagua njia sahihi.

Naomba nikukumbushe kwamba bado dunia inakutazama yale uliyosema utafanya bado wanaakuchungulia kama ni kweli yatatokea au lah. Kama utakubali kukata tamaa utakuwa umewathibitishia wale waliosema kwamba huwezi, utashindwa, umepotea.

Kama hutokubali kushindwa ukaendelea mbele hadi ndoto yako ikatimia utakuwa umewafunga mdomo wale waliosema huwezi. Wale waliokutia moyo watafurahi pamoja na wewe na kukupa hongera.

Ombi langu kwako usikubali kujiangusha wala kuwangusha tuliokutia moyo. Tuliosema unaweza bado pia tunakutazama. Usitufanye tuone tulikwambia uongo. Endelea kusonga mbele waliosema huwezi wafunge mdomo.

 

Kitu cha ajabu ni kwamba wale waliokukatisha tamaa hawawezi kukusaidia chochote Zaidi ya kukutazama tu. Ukipitia changamoto ukakosea ukaenda kuwaomba msaada. Wataishia kukwambia tulikwambia biashara ngumu aisee. Achana na hayo mambo, ona sasa umekuja kuomba tena pesa.

Watu hawa usikubali hata siku moja kwenda kuwaonyesha una shida. Watu hawa hawawezi hata siku moja kuwashauri wengine waje wanunue kwenye biashara yako lakini wako tayari kukusema vibaya. Watu hawa wakija kununua kwenye biashara yako wanakuja tu kukutazama unaendelea au umefilisika wapate cha kusema.

 

Watu sahihi wa kuwaeleza matatizo na changamoto unazopitia ni wale waliokushauri vyema. Wale ambao wanaweza hata kuwaambia wengine juu ya kile unachokifanya ile upate wateja Zaidi. Hawa ndio watu ukikwama unaweza kuwaendea na wakakusaidia hata kwa mawazo na hatua za kuchukua.

Usisahau dunia inakutazama. Waliokuvunja moyo wanatamani ushindwe ili utabiri wao utimie, tuliokutia moyo tunatamani ufanikiwe ili tufurahi.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading