Habari rafiki. Kitu ambacho hupaswi kukisahau ni kwamba hapa duniani ipo siku utaondoka. Na kitu cha kukumbuka Zaidi ni kwamba utaondoka peke yako.
Wale wote uliokuwa unawaonea aibu, unaona kwamba watakusema vibaya, wataona umejishusha hadhi kwa kufanya kile unachokitaka hutaondoka nao. Inawezekana ukawaacha duniani au wakakutangulia.
Sasa nikwambie rafiki hii ni dunia kila mmoja alikuja kivyake na kila mmoja ataondoka kivyake. Achana na watu unaodhani unawaogopa watakudharau wakati unazaliwa pengine hawakujua hata kama umezaliwa.
Chukua hatua sasa anza kufanya kile unachotaka, anza kuitimiza ndoto yako. watakuonaje wewe ukiwa unawakopa pesa ili uendeshee Maisha yako?
Kama unaogopa watakuonaje ukianza biashara embu jiulize watakuonaje ukienda kuwalilia shida? Kama unaogopa watakuonaje ukifanya kitu unachoona kimedharaulkika unafikiri watakuonaje wakisikia una madeni ya benki nyumba inataka kuuzwa?
Maisha yako ni yako utaondoka peke yako. hao unaowaogopa marafiki, wafanyakazi wenzako, mliosoma pamoja hawana cha kukusaidia kama unawaogopa. Ukizidiwa sana wakijua wataanza kukusema. Kama ni kweli wanakujali basi wangekushauri kitu bora cha kufanya.
Maisha yako yaisiendeshwe kwa maoni ya watu wa nje wanaokutazama. Maisha yako yandeshwe na mipango yako, maono yako, kusudi lako, malengo na ndoto zako kubwa. Usikubali maoni ya watu yakawa ndio muongozo wa Maisha yako. kuna siku itafika hutawaona tena hao unaowaogopa au utakuwa mwenyewe kwenye kaburi ukijutia aina ya Maisha uliyoishi hapa duniani.
Rafiki yangu hakuna Maisha mabovu kama ya kuishi huku unaangalia wengine watasema nini. Unakuwa unaishi Maisha ya kuwaridhisha watu ambao hata hawana msaada wowote kwenye Maisha yako.
Chukua hatua sasa usiogope watasema una elimu kubwa unafanya hiyo biashara? Kama huna hela ni huna hela tu kiwango cha elimu hakileti hela mfukoni. Ondoka hapo ulipo anza kile unachoweza ili ndoto yako itimie.
Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/
Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”