Watu wengi huja kwenye Maisha yetu wakiangalia ni kitu gani watapata na ndio maana mara nyingi ukiwa huna chochote huwezi kuwa na watu wengi waliokuzunguka.

Natamani wewe usiwe kama watu wa aina hii. Embu nenda kwenye Maisha ya wengine ukiwa na kitu cha kuwapa. Kila mtu ana kitu cha kutoa kwa wengine.

Kinachotuzuia ni Ubinafsi. Unaajiangalia wewe kwanza utapata nini kwa mtu huyu wakati huo huo unasahau kwamba na yeye inawezekana anakuangalia una kitu gani cha kumpa.

Tengeneza Thamani yako, ili ukikutana na watu wasitamani uondoke kwenye Maisha yao. Uwaachie alama ambayo ukiondoka watakukumbuka na kukuita tena.

Sijasema uwe unatoa bure vitu ambavyo Mungu amekupa, bali tafuta angalau kitu kimoja au viwili ambavyo ukivitoa kwa wengine wewe hutapata upungufu wowote lakini bado utakuwa umeyaongezea Thamani maisha yao.

Nakukumbusha, Jifunze Kila Siku hii ndio njia rahisi ya wewe kuongeza Thamani yako.
Soma Vitabu, soma Makala Kama Hizi.
Naamini na mimi nimeongeza kitu kwenye Maisha yako leo.

Ubarikiwe sana.

Unahitaji Blog/Website? Tembelea www.netpoa.com ufanye kazi nami.

8 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading