HATUA YA 299: Kama Unafanya Hivi Umeshatoka Nje ya Kusudi.

jacobmushi
2 Min Read

Ikifika mahali kila unachokifanya hutaki kusikiliza wengine, kushauriwa wala kukosolewa ujue kwamba unalolifanya umeshapotea njia. Hii ni kwasababu karibu kila tunalolifanya hatufanyi kwa ajili yetu bali kwa ajili ya wengine. Haijalishi wewe una kipaji kikubwa kiasi gani unaimba vizuri sana haujiimbii wewe mwenyewe unaimba ili watu wasikie kile unachokitoa.

Kama umefikia sehemu ambayo wale ambao unafanya kwa ajili yao hutaki kuwasikiliza wala kujua unachopeleka kinapokewaje unakuwa kama unafanya kwa ajili yako na sio kwa ajili ya wengine.

Maisha yako hapa duniani na kila kitu ambacho unacho cha pekee sio kwa ajili yako ni kwa ajili ya wengine. Kama unafikia sehemu ambayo unaanza kuwadharau watu ambao wamekuwa sababu ya wewe kufika huko juu ulipo unakuwa unapoteza maana ya kile unachokifanya.

Haijalishi uliweka bidi kubwa kiasi gani wakati unaanza bado kuna nguvu ya watu wengi unaowajua na usiowajua ilihusika kukuwezesha wewe kufika hapo ulipo. Maisha yako ni kwa ajili ya wengine waheshimu wengine jali Maisha ya wengine, tenda wema kwa wengine.

Ukiona umeshaanza kusahau juu ya watu na kujifikiria wewe mwenyewe ujue umeshatoka nje ya kusudi.

Ukiona umeanza kupata kiburi na hata hutaki kukosolewa ujue umeshatoka nje ya kusudi.

Ukiona unafika sehemu unawaona wengine sio chochote basi ujue umetoka nje ya kusudi.

Kuwa na muda wa kuyatafakari matendo yako kila wakati usije kujikuta umeshahama kwenye mstari. Kuna mambo tunafanya mengi yasiyo na msingi wowote kwenye Maisha ya wengine bali kwa ajili ya tamaa zetu.

Maisha yako yamebebwa na Kusudi, ukiliacha kusudi maana yake umeyapoteza Maisha yako.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading