“If you want to make a permanent change, stop focusing on the size of your problems and start focusing on the size of you!” T. Harv Eker

Harv Eker Mwandishi wa Kitabu cha The Secret on the Millionaire Mind anasema ukitaka kuleta mabadiliko ya kudumu acha kutumia nguvu nyingi kwenye ukubwa wa matatizo yako na uanze kubadilisha wewe uwe mkubwa Zaidi ya matatizo yako.

Yaani ni kwamba matatizo mengi tunayopitia yanasababishwa na ule uwezo wetu mdogo tulio nao juu ya matatizo yetu. Kuna mambo ambayo unayatia wewe unaona ni magumu lakini kwa mwingine ni rahisi sana kwasababu alishavuka hapo amekua Zaidi yako.

Ugumu wa Maisha yako unasababishwa na udogo wa uwezo wako wa kutatua matatizo. Ukitaka kuleta mabadiliko ya kweli na ya kudumu anza na wewe kwanza.

Unaweza kuleta mabadiliko ndani yako kwa kuanza kubadilisha uwezo wa kufikiri, badilisha au kuza uwezo wako wa kutengeneza kipato. Jifunze kwa wengine ambao wameshapita hapo ulipo wewe.

Kwa kawaida kama kuna jambo linakusumbua ukweli ni kwamba lilishawahi kumsumbua mtu mwingine na akalishinda. Hivyo tafuta kujua wengine walipitaje hapo ulipo.

Kama unasumbuliwa na madeni achana na madeni ingia ndani yako jitengenezee nidhamu ya matumiz ya pesa. Badala ya kukazana kulipa madeni hakikisha unaongeza uwezo wako wa kutengeneza kipato na ujitengenezee tabia ya kutumia fedha kwa nidhamu.

Yapo matatizo mengi ambayo yanakuwa magumu Zaidi kwasababu tu tuna uwezo mdogo wa kufikiri juu ya matatizo yetu.

 

HAKIKISHA UNAKUWA NA KUONGEZEKA KILA SIKU, SOMA VITABU NA MAKALA, JIFUNZE KWA WATU AMBAO WAMEPIGA HATUA ZAIDI YAKO. KUWA MDADISI JUU YA NAMNA YA KUTATUA MATATIZO MBALIMBALI.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading