Sifa ya binadamu ambayo tumejijengea na ni kubwa sana ni pale kujenga mazoea Fulani na mazoea yale yanakuja kuwa tabia zetu. Na siku zote mtu anapokizoea kitu anaweza kukichukulia cha kawaida sana na asikipe tena thamani yake. Unapotaka kuwa na bidhaa ambayo watu watahitaji sana kwenye maisha yao na wasiipate mahali kwingine unakuwa umejijengea namna ya kupata wateja ambao utadumu nao sana.

Kitakachokusaidia wewe udumu na wateja wako kwa muda mrefu ni pale unapokuwa na kitu cha pekee ambacho hawawezi kukipata mahali pengine. Bahati mbaya sana biashara unayoifanya kuna mtu mwingine anaweza kuja kuanzisha kama hiyo tena hapo jirani yako kabisa. Kama utakosa kitu cha kukutofautisha utajikuta hakuna mteja atakaeendelea kuja kwako.

Kitu kinachokutofautisha ndio kinaweza kuwa sababu kuu ya wewe kudumu sokoni na kufikia mafanikio bila ya kusumbuana na washindani wako. Mpe sababu mteja wako ya kuendelea kuja kwenye biashara yako tena na tena. Mpe sababu ya kukumbuka na kuwaambia wengine anachonufaika nacho kwenye biashara yako.

Utofauti wako unaweza kuwa ni namna unavyowahudumia kwa ukarimu sana na furaha. Utofauti wako unaweza kuwa ni uchangamfu wako hasa pale unapoulizwa maswali.

Utofauti pia unaweza kuwa ni ubora wa huduma au bidhaa yako. Inawezekana kuna vitu vya ziada ambavyo mtu anapata akija kwenye biashara yako.

Ukishamfanya mteja aone vitu vya tofauti unatakiwa uongeze bidi kiasi kwamba mteja awe tegemezi kwenye biashara yako. Awe hajisikii sawa asiponunua kitu kwenye biashara yako. Na hapa sizungumzii uwe mchawi bali uwe na vitu vya kipekee sana kuliko wengine.

Mfanye mteja atabasamu hata kama huko kwao amekuja akiwa amenuna.

Nimewahi kukutana na watu wengi wakisifia sehemu Fulani za biashara kwasababu ya lugha nzuri inayotumika wakati wa kuongea na mteja. Unachokifanya sasa hivi kinaweza kisiwe na matunda kwa wakati huu lakini unapanda mbegu ambayo itadumu kwa muda mrefu sana.

Kama ilivyo asili ya binadamu anapenda kufanya mambo aliyozoea na kutegemea sehemu Fulani ndivyo inavyotakiwa iwe kwenye biashara yako. Usikubali kumhudumia mtu akiondoka ndio basi. Tumeshapitwa na hizo zama tupo kwenye kipindi kingine ambacho ni lazima ulete utofauti kwenye soko.

Tafuta kwa bidii kinachokutofautisha kwenye biashara unayoifanya. Kwasababu hicho pekee ndio kinamfanya mtu aendelee kuwepo kwenye biashara mengine yote yatakuwa hayana maana kama wengine wanaweza kufanya.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading