Kuna aina Fulani ya maisha ambayo mara nyingi unapenda watu wajue kuwa unayo au unayaishi lakini katika uhalisia hauishi maisha hayo. Ni kwekli sio sawa kuonyesha kila kitu wazi kwenye dunia lakini ni vyema sana yale maisha ambayo unataka watu waone na wajue kuwa unayaishi ukaanza kuyaishi kiuhalisia badala ya kujifanya.
Ukiendelea kujifanya kuwa una maisha Fulani lakini uhalisia ni mwingine utaendelea kuteseka tu na kuwadanganya wengine. Kama kuna tabia unataka watu waone uko nazo acha kuigiza ziishi hizo tabia.
Kama wewe sio mwaminifu unataka watu wajue wewe ni mwaminifu acha kuigiza uaminifu anza kuishi uaminifu.
Kuendelea kuonyesha vitu ambavyo ni tofauti kabisa na uhalisia wa maisha yako ni kuendelea kujitesa na kujidanganya mwenyewe. Hawa unawaonyesha huku nje wala hawajali sana yale maisha yako.
Kama kuna tabia unapenda watu wajue kwamba ni zako halafu katika uhalisia una tabia nyingine kabisa huko ni kujitesa tu. Chagua moja ishi zile tabia unazozificha bila kujidanganya ama anza kuishi zile tabia unazotaka watu wajue kuwa uko nazo.
Hakuna haja yeyote ya kuishi maisha ambayo ni uongo na ukiujua ukweli kwamba unawadanganya watu. Anza sasa kuishi kile unachotaka watu waone kwenye maisha yako na acha maigizo.
Wewe halisi ni yule ambaye hakuna anaekuona huyu mwingine ni maigizo kama ni tofauti na yule ambaye ukiwa peke yako. Kama upo kwenye mahusiano halafu kuna tabia Fulani unataka mwenzako ajue unazo lakini kiuhalisia hauna ni kujitesa tu.
Wakati ulionao ni sasa anza kuishi maisha yale unayotaka watu wajue kuwa unayaishi badala ya kuigiza. Anza kutengeneza zile tabia ambazo unapenda watu waone unazo badala ya kuigiza. Anza kufanya vile vitu ambavyo unataka kila mtu aone unafanya badala ya kuigiza.
Utakuwa unajidanganya mwenyewe na kujitesa kama utakuwa na maisha ya aina mbili ya hadharani na ya sirini. Kuwa mtu mmoja kuwa na maisha ya aina moja na hapo ndipo tunaweza kusema kwamba wewe uko huru.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”