I never did anything worth doing by accident, nor did any of my inventions come by accident; they came by work. Plato

Sijafanya kitu chochote kilicho cha thamani katika kufanya kwa ajali, wala hakuna uvumbuzi wangu uliokuja kwa ajali; vyote vilikuja kwa kufanya kazi. Plato

Hii inatuonyesha kwamba chochote kile ambacho unafikiri kina thamani kubwa kwenye Maisha yako ili ukipate lazima uweke kazi kwa bidii. Hakuna muujiza wala bahati nasibu kwenye kupata vitu vya thamani kama Ndoto yako na maono yako.

Achana na Imani za kulala maskini na kuamka ukiwa umejishindia kitita cha pesa vitu hivyo haviwezi kudumu kwasababu havina nguvu yako uliyoweka.

Tambua kwamba Ndoto yako ili itimie inahitaji kazi kwa bidii na juhudi Zaidi.

Chochote kile chenye thamani hakitokei chenyewe kwenye Maisha yako lazima wewe uhusike katika mchakato wa matokeo.

Rafiki yangu mafanikio sio kuongea ni kutenda kwa kuweka kazi. Amua kufanya kazi kwenye kile unachokipenda hadi kikuletee matokeo yale unayotaka.

Maisha hapa duniani yanapimwa kwa kile ambacho umekifanya. Thamani ya kile unachokifanya inapimwa kwa matokeo unayopata.

Usiogope songambele weka juhudi Zaidi ili uweze kufikia maono yako.

Yatazame Maisha yako leo ni kitu gani kinakupa sababu ya kuendelea kuishi? Ni kitu gani kinakufanya uone bado unatakiwa kuwepo duniani? Kifanyie kazi kitu hicho hadi kilete matokeo unayotaka.

Ndoto Yako Inawezekana.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Usiishie Njiani

Timiza Ndoto Yako

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading