Penda kujipa muda wa kusubiri matokeo unayoyataka wakati unayafanyia kazi. Bahati mbaya hatuna kipimo maalumu cha muda ili uwe na uhakika wa unachokisubiria. Kama mwanamke amebeba ujauzito inafahamika kabisa ni baada ya miezi tisa atajifungua. Na endapo itatokea tofauti na hapo muda ukizidi tunaanza kupata wasiwasi. Kwenye mafanikio hakuna mahesabu ambayo yapo na uhakika kabisa kwamba ukifanya kitu Fulani baada ya muda Fulani utapata matokeo Fulani. Matokeo yanaweza kuwa makubwa Zaidi au yasifike hata nusu ya ulivyoambiwa.

Unachopaswa kutambua ni kwamba hauwezi kupata matokeo nje ya mchakato. Haiwezekani ukataka mtoto lakini hutaki kubeba ujauzito. Haiwezekani unataka mafanikio huku unakwepa gharama, hutaki kulipa gharama zinazotakiwa ili upate matokeo yanayohitajika. Hujajitoa vya kutosha unataka matokeo makubwa. Unafanya mambo ya hovyo lakini unataka matokeo bora.

Haijalishi umeumizwa kiasi gani na hasara uliyopata kuharibika kwa mimba sio mwisho wa kubeba nyingine. Hadi pale madaktari watakaposema huna uwezo wa kubeba ujauzito tena ndipo mtu anapokata tamaa na kubakia akisubiri muujiza. Sasa wewe unakataje tamaa wakati hakuna uthibitisho wowote unaosema kwaba haiwezekani tena?

Pamoja na kushindwa au kupata hasara huko unakosema umeshajaribu mara ngapi?

Umejifunza vitu gani kwenye kila jaribio uliloshindwa?

Inawezekana unalalamika kushindwa lakini nikikuuliza umejifunza nini utanijibu hakuna. Kama hakuna ulichojifunza unapaswa kurudia tena. Kama umejifunza pia rudia tena lakini usirudie makossa ya mwanzo. Kuanza ni kitu kingine na kufika mwisho mkubwa na kile ulichoanza ni kitu kingine. Watu wengi huishia katikati.

Unapoona ugumu unakuja ujue ndio ushindi umekaribia, mama mjazito anapokaribia kujifungua ndipo hupata maumivu makubwa ya uchungu. Sasa kama uchungu utakuja halafu wewe ukate tamaa utakua umeua kiumbe hai ambacho kilikuwa kizaliwe. Unapokimbia changamoto tambua kwamba umeua vitu ambavyo vingezaliwa baada ya changamoto uliyokuwa unapitia.

Unapokata tamaa katikati ya safari unafanana na binti ambaye ametoa ujauzito wake ili aendelee kubakia msichana. Kwasababu una hali Fulani uliyoizoea labda ni mshahara au sehemu ambayo mahitaji yako yalikuwa yanatimizwa unajikuta haupo tayari kujitoa ili upande viwango vingine unakata tamaa haraka.

Usikubali kubakia hivyo ulivyo hivi unajua binti akichelewa kuolewa umri ukaenda sana anasumbuka kupata wa kumuoa? Na wewe pia ukibakia hivyo ulivyo unatakiwa ujue mambo yanabadilika kama wewe hutabadilika kuna nyakati zinakuja hapo ulipo hapatafaa tena itakubidi usonge mbele na kwasababu ulipoteza muda hapo gharama kubwa itatakiwa ili uweze kupanda viwango vingine.

 

SONGA MBELE USIISHIE NJIANI. UMEZALIWA UWE MKUU. NGUVU UWEZO NA KILA KITU KIPO NDANI YAKO.

USIKUBALI KUBAKI NYUMA DUNIANI INABADILIKA NA WEWE KIMBIA NA MABADILIKO.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading