Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umeshajifunza kitu chochote leo? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu?
Mambo madogo madogo tunayofanya kila siku ndio yanatuletea ushindi mkubwa. Hivyo ni muhimu sana unapoyafanya uyafanye kwa umakini na ubora wa hali ya juu.
Ili usiishie njia unaweza kutumia mbinu ya kukomaa kwenye jambo uliloamua kilifanya hadi upate matokeo au ufikie mwisho. Maisha tunayoishi kipindi hiki yana muingiliano mwingi sana kiasi kwamba watu wanashindwa kufanya mambo kwa ufanisi na ubora.
Unaweza kuanza kufanya jambo Fulani mara simu inaita, au umechukua simu unaanza kupekua mitandaoni mwisho wa siku unapoteza mwelekeo wa kile unachokifanya na unashindwa kukifanya vizuri.
Ili uweze kuwa na matokeo bora wakati umeamua kufanya jambo Fulani labda ni kuandika hakikisha umeandika mpaka umemaliza ndipo uendelee na vitu vingine. Unapofanya kidogo kisha ukaacha na kwenda kuangalia vitu vingine unapoteza nguvu na unakuja kuwa mvivu wa kumalizia kazi yako.
Unapoweka mawazo yako yote sehemu moja unapata uwezo wa kufikiri kwa ubora na kuleta matokeo mazuri. Unapojichanganya unakosa nguvu ya kufikiri sawasawa. Ni sawasawa na computer ambayo umefungua mafaili mengi kwa wakati mmoja mara nyingi huzidiwa na mwisho wa siku unashindwa kuendelea na kazi nyingine.
Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/
Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”