Kama alikuumiza kisha akaondoka hakuwa wako. Au tunaweza kusema muda wake wa kuendelea kuwepo kwako ulifika na njia ya kuondoka kwa ilikuwa lazima wewe uumie kwasababu haukujiandaa kuondoka kwake.

Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

1 YOHANA. 2:19

Ni kweli umeumia sana, ni kweli ulikuwa na matarajio mengi sana juu yake. Ni kweli ulizijenga picha mbalimbali za maisha yenu ya baadae, ila sasa ndio ameshaondoka.

Huwezi kulazimisha kubaki kwako, ni wakati wake umefika sasa na imembidi aondoke kwako.

Unapaswa kukubali kwamba mtu huyu ni kweli nilimpenda sana lakini napaswa kumwacha aende. Napaswa kumuondoa ndani ya moyo wangu ili na mimi niweze kusonga mbele na maisha yangu.

Hutaweza kuendelea mbele vyema huku ndani ya moyo wako umewabeba watu ambao walishaondoka kwenye maisha yako. Yakupasa uwatue kwanza ndipo uweze kupata nguvu na wepesi wa kusonga mbele kwenye safari yako.

Ni kweli mambo yaliyotokea yamekuumiza sana, kila unapoyatafakari unajikuta unatokwa na machozi. Naomba ukumbuke kwamba pamoja na hayo bado maisha yanatakiwa yaendelee.

Bado unatakiwa kuishi maisha yako. Bado unatakiwa ulitimize kusudi lako hapa duniani. Hivyo basi ni wakati wako kukubaliana na hayo yaliyotokea kisha usonge mbele na safari.

Kama aliweza kuondoka basi hakuwa wako, kama angekuwa wako angevumilia. Kama angekuwa wako asingekubali kusikiliza maneno ya watu, Kama angekuwa wako angeweza kukusubiri.

Soma: Ukiachwa Ni Nani Anakuwa Amepoteza?

Sasa usihangaike kujifikiria eti wewe una tatizo gani wewe huna tatizo lolote ni kwamba tu yeye hakuwa wa kwako.

SIMAMA JIKAZE, SAFARI BADO INAENDELEA.

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading