Category Archives: AFYA, HEKIMA NA UTAJIRI

S1E12: Penda Tatizo Unalotatua.

By | October 2, 2019

Nipo natazama nyimbo YouTube nimekutana na wimbo uliwekwa mwaka 2009. Huo wimbo kwa mimi kuutazama leo pamoja na wengine wengi huyo mwimbaji atalipwa na YouTube (Google) mamilioni ya pesa. Nilichojiuliza ni kwamba huyu mwimbaji wakati anatunga wimbo huenda hakuwahi kuwaza kama mwaka huu 2019 huo wimbo wake bado ungeendelea kuingizia pesa. Nataka niseme na wewe unaefanya kitu chako… Read More »

S1E11: Atawainua Kunguru Wakulishe.

By | September 6, 2019

1 Wafalme 17:4,6 [4] Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. 6. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. Nimewatafakari wale Kunguru waliomlisha Elia nyama na mkate tena kipindi ambacho nchi ilikuwa imekosa mvua karibu miaka mitatu (maana yake kulikuwa na njaa) nikagundua Mungu anaweza… Read More »

S1E10: Yanapotokea Usiyoyatarajia.

By | September 4, 2019

Ni kweli mtu unaweza kuwa na fikra hasi juu ya Maisha yako lakini hakuna mtu hata mmoja anaetaka zile fikra hasi zitokee. Kinachomfanya mtu ajikute anawaza sana ni kwasababu ya hofu. Kila mtu huogopa pale anapowaza mambo mabaya yatatokea siku moja, kila mmoja anaweza kusita kuchukua hatua pale anapohisi kuna jambo baya litatokea kwenye kile anachotaka kufanya. Maisha… Read More »

S1E9: Nilimwona Akiingia Gesti Jana Jioni

By | August 24, 2019

Ni mara ngapi umewahi kuambiwa kuhusu wengine, mfano; “Nilimwona Fulani akiingia Gesti Jana”, “Fulani ana Mwanamke Mpya” na mengine mengi. Ukweli ni kwamba huenda umeyasikia sana kutoka kwa watu au hata wewe ulishawahi kumwambia mtu. Sasa nikwambie kitu kimoja, hayo ni maoni tu ya watu ambayo hayana ukweli halisia. Ngoja nikupe kisa hiki, Miaka michache iliyopita nilikuwa na… Read More »