Furaha itakuja pale ambapo utaanza kuishi Maisha ambayo moyo wako unataka na sio vile ambavyo watu wanataka uishi.

Furaha ya kweli ipo ndani yako na utaweza kuipata kwa kuishi kile ambacho Mungu ameweka ndani yako.

Hakuna haja ya kuishi Maisha vile ambavyo jamii inakulazimisha wewe uishi, vile jamii ambavyo imetengeneza na kutoa maana ya Maisha.

Utaona kwamba tumejengewa kuwa mafanikio ni kuwa na gari au kuwa na muonekano Fulani (wengine wanasema ukiwa na kitambi basi una pesa) lakini ukweli upo ndani yako.

Kile ambacho kinakupa wewe amani ya moyo ndio ya kweli na sio kile ambacho ukifanya kila mtu atakusifia na kukupongeza.

Ukifanya jambo au ukiishi Maisha ambayo kila mtu anakupa pongezi lakini wewe binafsi hufurahii hayo Maisha au hilo jambo haina maana yeyote.

Ishi kile ambacho moyo wako unataka, fanya kile ambacho kinaleta amani na furaha ndani ya moyo wako.

Fedha na mali za dunia hii ni matokeo ya wewe na moyo wako kuridhika na kufurahia kile ambacho unakifanya.

Endelea mbele, endelea kuamini kile unachokifanya sasa kama tu kinatoka ndani ya moyo wako. Wapo watu watakupinga, watasema unapoteza muda, utachelewa sana, lakini wewe binafsi ndio unajua unapokwenda na nini unataka.

Tengeneza maana yako ya mafanikio na aina ya Maisha unayotaka uanze kuyatengeneza. Achana na tafsiri za wengine. Achana na maana za wengine, kama wao wanapambana wanunue magari ya kifahari na kujulikana sio kwamba wewe haupo sawa au haupo sahihi kwasababu hutaki vitu hivyo. Wao wanaweza kuwa sahihi na wewe pia uko sahihi kwasababu moyo wako ndio unataka hicho unachokipigania.

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

4 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading