BARUA MAALUMU KWA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAOA AU KUOLEWA.

Habari za leo Rafiki, ni matumaini yangu kila mmoja anaendelea vyema kwenye Maisha yake na kupambana ili kupata matokeo bora Zaidi. Nina Imani kabisa unalifahamu kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Hujazaliwa kwa bahati mbaya, kila mwanadamu amekuja na uwezo ambao anatakiwa autumie hapa duniani ili aweze kuishi Maisha bora na yenye mchango kwa wengine […]

UJUMBE WANGU KWAKO KIJANA MWENZANGU

Vijana ndio tegemeo kubwa katika sehemu mbalimbali za kijamii, kidini, n ahata pia kisiasa. Kwenye serikali tuna maaskari polisi wengi ambao ni vijana pamoja na wanajeshi. Dini zetu pia zinahitaji vijana Zaidi kwasababu ndio pekee wenye nguvu kuliko wazee na watoto. Vijana pekee ndio wanaweza kufanya mambo makubwa na yakaleta matokeo makubwa. Vijana ndio wanahusika […]