HATUA YA 310: Ni Kama Kivuli Tu.

Maisha Yako yaliyokwisha kupita ni kama kivuli nyuma yako. Sio kila mtu anaekutazama ataweza kuona kivuli chako labda awe alishakuwa nyuma yako. Unachotakiwa kujua ni kwamba kivuli hakiwezi kuondoka hasa unapokuwa kwenye mwangaza. Pamoja na kuwa kivuli chako kinaendelea kukufuata hakitakiwi kiwe sababu ya wewe kushindwa kusonga mbele. Ni kweli kuna vivuli vingine vinatisha sana […]

HATUA YA 305: Wakati Wako Upo.

Haijalishi unapitia hali gani sasa, unapaswa kujipa moyo na kujitia nguvu kwasababu wakati wa wewe kufanikiwa na kuinuka kwenda viwango vingine upo. Unaweza kupambana sana na kutumia kila njia ambazo unafundishwa na unazosoma kwenye vitabu lakini ukajishangaa kwamba hakuna mabadiliko yeyote. Unapaswa kuendelea kujipa moyo kwamba hautabaki kama ulivyo milele. Asubuhi yako inakuja usitishwe wala […]

#USIISHIE_NJIANI:  ONA VITU KABLA HAVIJATOKEA.

Ili uweze kupata chochote unachokitaka lazima uanze kuona kwenye akili yako kabla hakijatokea kwenye uhalisia. Anza kutengeneza picha ndani ya fikra zako ndipo utaweza kupata kwenye uhalisia. Hakuna kitu kinatokea chenyewe kwenye maisha yako kama ajali lazima uanze kutengeneza picha na uifanyie kazi picha hadi itokee. Unajua muujiza unatokea bila ya sisi kutarajia au pale […]

#USIISHIE_NJIANI- Kujionyesha na Uhalisia.

Haina maana yeyote kama watu watajenga picha kubwa kwako kutokana na namna unavyopenda kujionyesha halafu uhalisia ukawa ni tofauti kabisa. Ni vizuri sana ukaishi vile unavyopenda lakini ni vyema ukakubali kulipa gharama za hayo maisha kwanza ndipo uje kufurahia baadae. Ni kichekesho sana kama utakuwa unatamani watu waone unaishi maisha mazuri wakati kwa ndani unateseka […]