Connect with us

483; Unapohisi Kama Mungu Amekuacha

MAFANIKIO MAKUBWA

483; Unapohisi Kama Mungu Amekuacha

Kumzuia mtoto asitembee mwenyewe kwasababu tu unaogopa ataanguka na ataumia sio kumsaidia ni kumlemaza.

 Hivyo ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku. Kuna vitu kama utaendelea Kuogopa kufanya au kutaka Kusaidiwa kila unapofanya unakuwa unalemaa.

Lazima ujifunze kufanya mwenyewe ili uwe na Ujasiri na kujiamini. Kamwe usifikiri Mungu amekuacha wakati wa magumu anataka ujifunze Kusimama Mwenyewe, sio kila wakati unaanguka hadi aje akuinue, kuna Wakati unaanguka na unatakiwa unyanyuke kwasababu una nguvu.

Mungu anakujua kuliko unavyojijua wewe. Anajua hapa unaweza hata kama wewe Unajiona huwezi.

Halafu hajakupa akili za bure sasa kama huzitumii akili haina maana ya kuwa nazo.

Endelea kumuomba, endelea kumshukuru, endelea kumshirikisha mipango yako. Kuna tofauti ya kumshirikisha Mungu mipango yako na kumuomba akusaidie kwenye mipango yako. Ukimchukulia Mungu kama baba yako basi utakuwa unamshirikisha Mipango yako. Unapokwama huwezi kuwa na wasiwasi wa kumrudia uombe msaada.

Ni ngumu sana kuja kumuomba baba yako mzazi pesa ukalipe madeni ya biashara ambayo ulianza bila kumshirikisha. Ni kweli atakusaidia ila ataona kama humheshimu hivi. Ila kama ulimshirikisha tangu mwanzo inakuwa rahisi sana kumwendea na kuomba msaada.

Mungu ni baba kwetu, tunapaswa kujijengea utaratibu wa kuzungumza nae kama baba yetu. Kumueleza mipango yetu, kumueleza malengo yetu hata kama tunaona tunaweza wenyewe. Yeye atatutazama kwa Karibu na ataleta msaada hata wakati mwingine hatujaomba.

Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

#usiishienjiani

www.jacobmushi.com

Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in MAFANIKIO MAKUBWA

To Top