“If you and I are having a single thought of violence or hatred against anyone in the world at this moment, we are contributing to the wounding of the world.” -Deepak Chopra
Kama mimi na wewe tukiwa na wazo moja tu la kuchukia mtu mwingine hapa duniani tunakuwa tunachangia vidonda/maumivu kwenye dunia.
Kuchukia ni sumu, huwezi kufurahia maisha ukiwa na chuki ndani yako. Bahati mbaya ni kwamba ukimchukia mtu wewe ndio unateseka zaidi.
Mtu akikutenda ubaya kuendelea kumchukia ni kuendeleza maumivu ndani yako. Ukiumia wewe hutaweza kuishi vizuri na waliokuzunguka. Wakati mwingine ile chuki unaweza kuanza kuisambaza na kuendelea kuharibu zaidi.
Jitahidi uwe na moyo mweupe, samehe, mwone mtu aliekutendea ubaya kama mtoto mdogo au aliechanganyikia, hii itakusaidia kupunguza mzigo wa chuki na maumivu.
Watu wanaotenda uovu hatupaswi kuwachukia tunapaswa kuchukia uovu wao. Huwezi kuondoa watu wote waovu duniani bali unaweza kutokuwa mmoja wao.
Nakutakia Kila la Kheri
Ubarikiwe sana
Rafiki Yako Jacob Mushi.