“Good people do not need laws to tell them to act responsibly, while bad people will find a way around the laws.” -Plato
Watu wema hawasubiri sheria iwaambie jinsi ya kuwajibika, wanajua majukumu yao na wanayatekeleza. Watu wabaya hata sheria zikiwekwa bado watatafuta namna ya kwenda Kinyume nazo.
Mtu mwema hasubiri ahamasishwe kuwajibika. Anawajibika mwenyewe.
Sheria zipo kwa ajili ya watu wanaozivunja. Mtu asievunja sheria haitaji sheria Kutekeleza kile kinachompasa.
Na Wewe Rafiki uwe mtu mwema. Maisha yako ni Majukumu yako, Mafanikio ni jukumu lako.
Kuishi na wengine vizuri ni jukumu lako. Kusamehe ni jukumu lako. Kufuatilia mambo yako ni jukumu lako.
Usisubiri mtu mwingine aje akuelekeze au akusimamie kwasababu utakuwa tayari umekwenda vibaya.
Wajibika kwa maisha yako.
Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana
Rafiki Yako Jacob Mushi.